Waziri Mkuu Awataka Wana-Lindi Kumchagua Dkt. Samia Oktoba 29 – Global Publishers



LINDI-Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Wana-Lindi wanakila sababu ya kumchagua Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,mwaka huu.

Amesema kuwa,Rais Dkt.Samia amegusa matamanio ya Wana-Lindi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa imegusa maisha ya kila siku ya wakazi wa mkoa huo.

Amesema hayo Septemba 13,2025 katika uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi mkoa wa Lindi na Wilaya ya Ruangwa zilizofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Likangala, Ruangwa mkoani Lindi.

“Tunayo sababu ya kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapinduzi, sote tunafahamu namna Rais Dkt.Samia alivyotekeleza miradi katika mkoa huu, kwenye sekta za elimu, afya, maji, barabara, uwezeshaji wananchi kiuchumi. Mkoa huu tunamiradi mikubwa itakayoufanya uchangamke na kuchachua uchumi wetu.”