Dar es Salaam. Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Na-tional League for Democracy (NLD), Doyo Has-san Doyo, ameahidi kuunda tume maalumu ita-kayounda ramani ya maeneo ya wakulima na wafugaji kwa kuweka mipaka ya haki kwa pande zote.
Doyo ameeleza hayo leo Jumatatu, Septemba 15, 2025, katika muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akihutubia wakazi wa vijiji vya Kijungu na Pori kwa Pori, Wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, Doyo amesema kwamba moja ya hatua atakazo-chukua akiwa Rais ni kuunda tume hiyo maalu-mu, kwa lengo la kutokomeza migogoro ya wakulima na wafugaji.

“Katika hili, ulinzi shirikishi utaimarishwa ili kuzuia migogoro ya mara kwa mara. Mkinipa ri-dhaa, sitavumilia kundi lolote litakalokiuka ma-kubaliano ya vikao vya kimila au Serikali,” am-esisitiza Doyo.
Mbali na tume, Doyo pia ameahidi kuweka aska-ri wa wanyamapori katika maeneo ya makazi ya watu, ili kusaidia kudhibiti tembo wanaovamia makazi na mashamba na kusababisha madhara makubwa kwa wananchi.
Aidha, ameahidi kutoa fidia kwa wananchi wote walioathiriwa na uvamizi wa tembo kama kifuta jasho kutokana na madhara hayo.

Doyo pia amewaahidi wananchi wa Kijungu ku-wa endapo atachaguliwa, Serikali yake itajenga hospitali ya kisasa katika eneo hilo ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma bora za afya, ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa wakazi wa Kijungu, kwa sasa hu-lazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya, kuelekea Kiteto Mjini au Songe katika Wilaya ya Kilindi, jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao, hasa katika hali za dharura.
“Nafahamu mnakabiliwa na changamoto nyingi, lakini changamoto ya afya inabeba msingi mu-himu katika ujenzi wa taifa.
“Ili tujenge taifa imara, tunahitaji wananchi wenye uhakika wa huduma za afya. Kuna haja ya kujenga hospitali hapa ili msilazimike kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu,” amesema.
Akizungumza kando ya mkutano huo, mkazi wa Kijungu, Hussein Said, amesema ahadi zi-nazotolewa na wagombea ni nzuri iwapo zitate-kelezwa.
“Doyo sio wa kwanza kupita hapa. Wapo wen-zake nao wamekuja kutuahidi na ahadi zao zi-naleta matumaini, lakini kuahidi ni jambo moja na kutekeleza ni jambo la pili,” amesema Said.