KOKA KULETA MAGEUZI MAKUBWA YA ELIMU NA AFYA KWA WANACHI KATA YA KIBAHA

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA 

Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha mjini kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka ameahidi kuboresha sekta ya afya,elimu na maji pindi atakapopewa ridhaa ya kuwaongoza  wananchi.

 Koka ameyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni za CCM kata ya Kibaha na kusema kuwa lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Koka amebainisha kwamba  anatambua wananchi wa kata ya Kibaha wanahitaji  kwa kiasi kikubwa huduma mbali mbali ikiwemo suala la   upatikanaji wa maji safi na salama.

“Kitu kikubwa ambacho ninawaomba kwa dhati  wananchi wa kata ya Kibaha ni kuniamini pamoja na kunipa kura ili niweze kuendelea kuwapatia maendeleo katika nyanja mbali mbali,”amesema Koka.

Kadhalika Koka amebainisha kuwa ataweka mipango madhubuti ya kuweza kuhakikisha anatengeneza na kuboresha miundombinu ya barabara.

Kwa upande wake Diwani mteule wa kata ya Kibaha Omary Bula  amesema kwamba dhumuni lake ni kusikiliza kero na kutatua changamoto za wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka amewaomba wanachama wa CCM pamoja na wananchi kumchagua kwa kura nyingi  za  kishindo  nafasi ya Rais Dkt.Samia,Ubunge pamoja na udiwani.