ADA COTTRELL FOUNDATION YATOA MSAADA NUNGWI-ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya ADA COTTRELL FOUNDATION kwa kushirikiana na Taasisi ya (LDF) Labayka Development Foundation imetoa mahitaji kwa Watoto wanaishi mazingira magumu katika kata ya Nungwi Wilaya ya Kaskazin A, Mkoa wa Kaskazini Unguja – Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurungezi Mwakilishi wa Taasisi ya Ada Cotterll Foundation Shedrack Albert amesema ugawaji wa mahitaji hayo ni muendelezo wa utaratibu unaofanywa kila mwaka ikiwa kama kumbukizi ya Mr Robert Cotterll kila ifikapo Agasti kwa kuwa ndio Mwezi aliofariki, Robart ambaye alikua ni Daktari nchini Marekani alifariki dunia agost 2028 akiwa na tatizo la Kansa.

Robert Cotter ameacha Mke Joyce Cotter na mtoto wa Kike Ada Cotter ambaye ndiye msimamizi wa Taasisi ya Ada Cottrell Foundation iliyopo nchini Marekani na tawi lake kwa sasa lipo nchini Tanzania

Amesema pamoja na ugawaji wa mahitaji hayo katika Visiwa vya Unguja bado vinakabiliwa na changamoto ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo bado wanahitaji msaada zaidi.

Akizungumza Khamis Juma Mtwana, kutoka taasisi ya Labayka Development (LDF) Foundation iliyopo Nungwi ameahidi kushirikiana na Taasisi ya Ada ameahidi kuhakikisha wanapunguza tatizo la watoto wenye uhitaji mjini humo.

Amesema pamoja na ugawaji wa mahitaji hayo pia imefanyika dua maalum ya kumuombea Robart cotter ikiwa kama kumbukumbu ya dua ambayo imeongozwa na Shekh Haji Ali,