Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya vinyozi watoa huduma katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameiadhimisha kwa kufanya matembezi ya hisani pamoja na usafi katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Mwanasheria wa Manispaa hiyo Steven Magala kwa niaba ya mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Frank Nkinda amesema Serikali inatambua mchango wa sekta hiyo muhimu ambayo inayotoa ajira kwa vijana huku akiwataka watoa huduma hao kupitia umoja wao kuendelea kushirikiana kwani Serikali ipo nao bega kwa bega.
Kwa Upande wake Katibu wa umoja wa vinyozi Wilaya ya Kahama Juma Diwani amesema maadhimisho haypo yalianza na matembezi ya amani kama sehemu ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kada hiyo sambamba na kufanya usafi kama sehemu ya kudumisha usafi.
Maadhimisho ya siku ya Kinyozi duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Septemba 16 ambapo kwa upande wa Wilaya ya Kahama yameongozwa na kauli mbiu isemayo, ‘Sekta ya vinyozi ni injini ya ajira kwa vijana, shiriki Uchaguzi mkuu’.

