▫️Jumla ya mapambano 21 kupigwa jioni ya leo
▫️Vilabu 15 kushiriki
MASHINDANO ya ngumi ya Klabu Bingwa ya Taifa yanatarajia kuanza rasmi jioni ya leo katika uwanja wa michezo wa Urithi, Jijini Tanga.
Jumla ya vilabu 15 kutoka mikoa ya Tanga, Dar es salaam, Kagera, Arusha, Iringa na Dodoma vinashiriki mashindano hayo vikiwa na jumla ya mabondia 97 ambavyo ni MMJKT, Ngome, Magereza, Polisi Arusha, Tanga Central, Tanga Central B, Makorora, Kagera Boxing A na B, Iringa Boxing Club, General Chande, Band Coy, JKT Mgulani, Jeba na Amboni.
Mabingwa watetezi timu ya MMJKT (JKT Makao Makuu) wamejitapa kuendeleza ubabe wao katika mashindano kwa kijisifia mafanikio yao ya kutwaa Ubingwa huo mara 4 mfululizo mbele ya mahasimu wao wa karibu timu ya Ngome.
Je Ngome watakubali ama vilabu vya Tanga na vingine kama Magereza na Polisi vitakaza?
Tufuatilie kupitia mitandao yetu ya kijamii mpaka fainali siku ya Jumamosi 20-09-2025 kujua Bingwa wa mwaka 2025 ni nani.
Matukio ya Klabu Bingwa ya Taifa ya mwaka 2024 yaliyofanyika Jijini Tanga.