Aliyekuwa Balozi wa Baba Mtakatifu (Vatican) katika nchi mbalimbali duniani, Mtanzania Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, amefariki dunia usiku wa Septemba 16, 2025 huko Roma, Italia.
Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa Oktoba 8, 1957 mkoani Kagera. Aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 6 Julai 1986 na Mhashamu Nestorius Timanywa, aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba. Tarehe 18 Machi 2010 aliwekwa wakfu katika Daraja Takatifu ya Uaskofu na Askofu Mkuu Tarcisio Pietro Evasio Kardinal Bertone, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Vatican.
Amehudumu kwa muda mrefu kama Balozi wa Baba Mtakatifu katika mataifa mbalimbali ikiwemo Angola, Honduras, Visiwa vya Fiji na kwingineko.
Related