Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Palamaganda Kabudi ndiye atazindua Mbio za Magari za Ubingwa wa Afrika 2025 ‘Mkwawa Rally of Tanzania’ keshokutwa Ijumaa, Septemba 19, 2025 mkoani Morogoro.
Ofisa Habari wa Mashindano ya Magari Tanzania, Michael Maluwe amesema kuwa maandalizi yote muhimu kwa tukio hilo la uzinduzi yameshakamilika.
“Madereva wameanza kuwasili Morogoro kwa ajili ya usajili na kuchukua nyaraka rasmi za mashindano. Alhamisi madereva watafanya ukaguzi wa njia (Recce) na ukaguzi wa magari (Scrutineering) katika makao makuu ya Mkwawa Leaf.
“Wasimamizi kutoka FIA tayari wamewasili nchini na wamekagua njia zote za mashindano, wakijiridhisha na maandalizi hususan suala la usalama,” amesema Maluwe.
Katika mbio za Afrika, pambano kubwa linatarajiwa kati ya Yassin Nasser na Samman Vohra, wanaowania taji la mwaka huu.
Madereva wengine pia wanakuja kwa nguvu kuwania nafasi tatu za juu.
Kwa upande wa Tanzania, huu ni mzunguko wa nne wa National Rally Championship (NRC) kuelekea kumpata bingwa wa taifa, kabla ya mzunguko wa mwisho utakaofanyika Novemba mkoani Arusha.
Bingwa mtetezi Manveer Birdi (Mitsubishi Evo 09) anakabiliwa na changamoto kutoka kwa kaka yake Randeep Singh (Mitsubishi Evo 09), Gurpal Sandhu (Mitsubishi Evo 10), na Ahmed Huwel (Toyota Yaris R5) ambaye analenga kutwaa ubingwa tena.
Washindani wengine wenye uwezo wa kuvuruga nafasi tatu bora ni, Shehzad Munge (Mitsubishi Evo), Samir Nahdi Shanto (Ford Proto), Altafu Mungu (Ford Fiesta R5) na Dharam Pandya (Subaru VAB).
Washindani kutoka mataifa mbalimbali ni pamoja na Hassan Alwi (Uganda), Akif Virani (Kenya) na Mohammed Roshanali (Burundi).
Mashindano haya yanatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa, hasa kutokana na idadi ya magari ya kisasa
Magari aina ya R5 (Toyota Yaris, Skoda Fabia, Ford Fiesta), Ford Proto–3 na Mitsubishi Evo X-3