RC MOROGORO ATAKA MAPINDUZI YA KILIMO KWENDA SAMBAMBA NA UBORESHAJI WA LISHE.

……………..

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema mapinduzi yaliyopatikana kwenye kilimo ndani ya Mkoa huo yanapaswa Kwenda sambamba na uboreshaji wa suala la LISHE ambapo kwa kiasi kikubwa bado ni changamoto Mkoani humo.

Mhe. Adam Malima ametoa wito huo Septemba 16, 2025 wakati wa kikao cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ngazi ya Mkoa kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Wilaya. 

Amesema, Mkoa wa Morogoro ndio Mkoa pekee katika Serikali ya awamu ya sita ulioitikia mapinduzi ya kilimo kuliko mikoa mingine hapa nchini  na kwa sababu hiyo amewataka watendaji wa Serikali Mkoani humo kuhusisanisha mapinduzi hayo ya kilimo kwenda sambamba na masuala ya lishe. 

“Nasema hivi kilimo na lishe viendane Pamoja, haya mafanikio tunayoyapata kwenye mapinduzi ya kilimo hebu tuyaoanishe na lishe” amesisitiza  Mhe. Malima. 

Hata hivyo amewataka viongozi ndani ya Mkoa huo kila wilaya kutumia fursa ya mazao yanayostawishwa katika eneo lao yawe chachu ya uboreshaji wa Suala la lishe katika eneo hilo. 

Katika hatua nyingine amewataka Maafisa lishe kuendelea kutoa Elimu kwa wazazi kuona umuhim wa Watoto kupatiwa lishe Bora mashuleni na kuchangia gharama zinazohitajika ili kuwawezesha Watoto wao kupata chakula kwa lengo la kuboresha uwezo wao kimwili na kiakili. 

Kwa upande wake Afisa Lishe Mkoa wa Morogoro Bi. Salome Magembe amebainisha bajeti ya lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kuwa zaidi ya Tsh. 970 Mil. zimetengwa kwa ajili ya lishe huku akifafanua uwepo wa ongezeko la utoaji wa fedha za lishe kutoka halmashauri za Mkoa huo kutoka asilimia 88 mwaka 2023/2024 hadi asilimia 94 mwaka 2024/2025. 

Pamoja na mafanikio hayo Bi. Salome amesema bado wanakabiliwa na changamoto ya mwitikio mdogo wa wazazi katika kuchangia chakula cha wananfunzi shuleni na ukosefu wa motisha kwa wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii jambo linalopelekea wahudumu kushindwa kutoa huduma stahiki kwa walengwa na kushindwa kuwafikia walengwa kwa wakati.

Aidha, amesema Mkoa wa Morogoro una mikakati ya kutatua changamoto z