………..
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amefanya ziara ya kitembelea ujenzi wa mradi wa shule maalum ya Sekondari ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja ujenzi na chuo cha ufundi Veta wilayani kigamboni sanjari na kufanya kikao na watendaji wa halmashairi hiyo na kuwataka kisimamia vyema ukusanyaji wa mapato ili kuboresha huduma za Jamii.
Akizungumza katika kikao cha viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo leo Septemba 17,2025 RC Chalamila amewataka watendaji kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha tedha hizo zinasaidia kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo Elimu na Afya huku akisisitiza suala la kuwa na miradi ya kudumu inayokidhi mahitaji ya miaka 30 hadi 50 ijayo
RC Chalamila amesisitiza suala la ujenzi wa miradi kwa mfumo wa ghorofa baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa chuo cha ufundi stadi Veta na kusema kuwa ujenzi wa chini hauzingatii matumizi sahihi ya ardhi hasa kwa jiji la Dar es salaam ambalo lina changamoto ufinyu wa ardhi kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu.
Akiwa katika mradi wa ujenzi wa shule maalumu ya Sekondari ya Mkoa wa Dar es salaam Chalamila amehimiza suala la uwepo wa madarasa yenye mfumo wa kisasa unaotumia TEHAMA kufundishia yaani Smart Classes yasiotumia chaki za kawaida.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Dalmia Mikaya amesema wilaya hiyo imeendelea kukusanya mapato kwa ufanisi na kusimamia vyema vyanzo vya mapato huku pia akimshukuru na kumpongeza Rais Dkt Samia kuiwezesha wilaya hiyo kupata fedha za ujenzi wa barabara za lami.