:::::::
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua rasmi Hatifungani ya Stawi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 150 ambapo kwanza itatumika bilioni 50, ikiwa ni mpango wa muda wa kati wa miaka mitano, kwa mara ya kwanza kuingia katika soko la mitaji nchini.
Hatifungani hiyo inalipa riba ya asilimia 13.5 kwa mwaka, ambayo italipwa kila baada ya miezi mitatu kwa wawekezaji. Fedha zitakazokusanywa kupitia hatifungani hii zitaelekezwa katika kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, kwa lengo la kuwasaidia kukuza biashara zao.
Akizunguzumza wakati wa uzinduzi wa hati fungani ya ‘STAWI’ Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya amesema hatifungani hiyo itawezesha kupanua wigo wa masoko ya mitaji sambamba na kupunguza utegemezi wa mikopo kigeni na hivyo kukuza ukuaji wa kiuchumi nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya TCB Adam Mihayo amesema hatifungani ya stawi itasaidia kutekeleza kikamilifu malengo ya benki kuwekeza katika teknolojia na ubunifu unaosaidia kufungua fursa za kiuchumi husisan kwa wafanyabiashara wadogo na wakati
Kwa upande wake na afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana CMSA Nicodemus Mkama wamesema hatifungani hiyo inalenga kukusanya shilingi bilioni 150 zitakazosaidia kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati