Halmashauri ya Mbulu Yatangaza Nafasi 4 za Dereva – Global Publishers



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi za kazi baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 4

Majukumu:

  • Kukagua gari kabla/baada ya safari.

  • Kuwapeleka watumishi safari za kikazi.

  • Kufanya matengenezo madogo ya gari.

  • Kutunza “Log Book” ya safari.

  • Kusambaza nyaraka mbalimbali.

  • Kufanya usafi wa gari.

  • Kazi nyingine kadri ya maelekezo ya msimamizi.

Sifa za Mwombaji:

  • Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV).

  • Leseni ya Daraja E au C.

  • Uzoefu wa angalau mwaka 1 bila kusababisha ajali.

  • Cheti cha mafunzo ya msingi ya Udereva (Basic Driving Course – VETA au chuo kinachotambulika na Serikali).

Ngazi ya mshahara: TGS B


Masharti ya Jumla

  • Awe Mtanzania mwenye umri wa miaka 18–45.

  • Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuomba na kuainisha aina ya ulemavu.

  • Kuwasilisha C.V yenye maelezo binafsi, namba za simu, barua pepe na majina ya wadhamini watatu.

  • Kuambatanisha nakala zilizothibitishwa na mwanasheria za vyeti vya elimu na taaluma.

  • Vyeti vya provisional, testimonials au statement of results HAVITAKUBALIWA.

  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na TCU, NECTA au NACTVET.

  • Waliojiuzulu/kuondolewa kazini Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

  • Mwisho wa kutuma maombi: 28 Septemba, 2025