Dkt. Mwinyi: CCM ni Mhimili wa Amani na Maendeleo

MGOMBEA wa kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduz (CCM), Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Wazanzibari kuendelea kukiunga mkono chama hicho akisisitiza kuwa ndicho mhimili wa amani ya Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo tarehe 17 Septemba 2025 katika Uwanja wa Kajengwa, Makunduchi, mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Mgombea wa kiti cha Rais wa Tanzania kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa wananchi wana kila sababu ya kuichagua CCM kwa maendeleo zaidi ya kijamii na kiuchumi.

Amehimiza wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa CCM.

📍 Leo, 18 Septemba 2025, mbio za kampeni zinaendelea Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Chagua CCM ✅
Chagua Dkt. Hussein Ali Mwinyi ✅
#UongoziUnaoachaAlama 
#HAM2025
#CCM2025