Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa
Sheria kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) Jamal Baruti wakati akizungumzia leo jijini Dar es salaam
kuhusu ukaguzi wa mazingira katika miradi ya maendeleo ambao unafanyika kwa
wiki nne iliyoanza tar 15 septemba hadi tar 12 Oktoba mwaka huu.
Meneja Kanda ya Kaskazin Mashariki Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC)Bi. Glory Kombe
(kushoto) akizungumzia leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi wa mazingira
katika miradi ya maendeleo ambao unafanyika kwa wiki nne iliyoanza tar 15 septemba
hadi tar 12 Oktoba mwaka huu
Onesmo Ndinga ni Afisa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Ufuatiliaji Sheria Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Hamadi Kisiwa akizungumza katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es salaam.
………………..
NA MUSSA KHALID
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC) linafanya ukaguzi wa mazingira katika miradi yote ya maendeleo Mkoani
Dar es salaam ili kuhakikisha miradi isiyokuwa na vyeti vya Tathmini ya Athari
kwa Mazingira inazingatia matakwa ya sheria na Kanuni za Mazingira.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu
Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria kutoka NEMC Jamal Baruti
wakati akizungumzia ukaguzi wa mazingira katika miradi ya maendeleo ambao
unafanyika kwa wiki nne kuanzia tar 15 septemba hadi tar 12 Oktoba mwaka huu.
Baruti amesema kuwa ukaguzi huo unafanyika kwa kushirikiana na
Ofisi za serikali za mitaa ili kuhakikisha miradi yote iliyopo katika eneo husika
inatambulika pasipo kuacha hata mradi mmoja.
Aidha ameuataja Mkoa wa Dar es salaam kuwa na hali
mbaya katika usimamizi wa mazingira kutokana na matumizi holela ya ardhi,
uchimbaji wa mchanga kwenye mito na mabonde, usimamizi hafifu wa taka ngumu na
changamoto ya taka za plastiki hali inayoathiri afya za watu na miradi ya
maendeleo.
Kwa upande wake Meneja Kanda ya Kaskazin Mashariki
Glory Kombe amesema kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana na
wenyeviti katika ukaguzi huo ili kuweza kuikagua miradi yote iliyopo kwenye
maeneo hayo.
Akizungumzia ukaguzi wa miradi ya Maendeleo, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Ufuatiliaji Sheria NEMC, Hamadi Kisiwa amesema zoezi hilo linahusisha miradi 300 kwa siku ambapo katika katika siku tangu tangu wameanza wametembelea miradi 900.
Onesmo Ndinga ni Afisa Sheria NEMC akizungumzia
adhabu zinazoweza kutolewa kwa wanaofanya uchafuzi wa Mazingira,amesema
kuwa BARAZA linaweza kutoa onyo lakini
pia kumtaka muhusika kurekebisha dosari zilizojitokeza kwa gharama zake.
Hata hivyo Mamlaka hiyo imewasisitiza Wakurugenzi wa
Halmashauri na kamati za Mazingira Hata hivyo Mamlaka hiyo imewasisitiza
Wakurugenzi wa Halmashauri na kamati za Mazingira kufuatilia miradi ya
Maendeleo ili kuhakikisha inazingatia taratibu za Mazingira.