Mtego nusu fainali Ligi ya KIkapu Dar

MACHO na masikio ni kwa miamba minne wa Ligi ya Kikapu Dar es Salaam (BDL) na zinasubiriwa mechi za kuamua timu zitakazotinga fainali, huku Dar City ikimenyana na Stein Warriors, huku Pazi ikikipiga na JKT kwa wanaume na kwa wanawake JKT Stars itacheza DB Lioness, huku DB Troncatti ikicheza na Jeshi Stars.

Nusu fainali hiyo iatakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, Mbuyuni, jijini Dar es Salaam, itapigwa kwa mfumo wa michezo mitatu na siyo mitano kama ilivyopangwa awali.

Katika mchezo wa kwanza kwa upande wa wanawake, utazikutanisha JKT Stars dhidi ya DB Troncatti kuanzia saa 8:00 mchana, kisha Jeshi Stars itaikaribisha DB Lioness kuanzia saa 10:00 jioni.

Kwa upande wa wanaume, Pazi itaumana na JKT kuanzia saa 12:00 jioni kabla ya Dar City kukutana na Stein kuanzia saa 2:00 usiku.

KIKA 02

Katika mchezo wa Stein dhidi ya Dar City, timu hizo zimetambiana kushinda, huku Stein ikipata sababu ya ushindi kutokana na mazoezi ya asubuhi na jioni ya kila siku ya nyota wake na mashabiki wanaofurika uwanjani kila inapocheza.

Timu hiyo ambayo inacheza ligi hiyo kwa mara ya kwanza, inajivunia wachezaji wake kama Brian Mramba, Evance Davies, Jonas Mushi, Mwalimu Heri, Felix Luhamba, Abasi Omari na Mwinyipembe Jumbe.

Dar City inajivunia uzoefu wa nyota wake wa kimataifa wakiwamo Sharom Ikedigwe, Clinton Best (Nigeria), Jamel Marbuary (Marekani), Victor Mwoka (Kenya), pamoja na wazawa Amin Mkosa, Fotius Ngaiza, Ally Abdallah na Hajee Mbegu.

Kocha wa timu hiyo, Mohamed Mbwana alisema kwa sasa lengo lao ni michuano ya kimataifa kwa maana ya kufuzu mashindano ya ubingwa wa Afrika;

KIKA 03

“Kwa sasa tunaangalia michuano ya mbele ya kimataifa ya kufuzu kucheza mashindano ya ubingwa wa Afrika BAL.”

Kwa upande wa mchezo wa Pazi dhidi ya JKT ambazo ni kongwe kwenye mchezo huo umeacha maswali kwa mashabiki, huku wengi wakiipa nafasi Pazi kutinga fainali.

Timu hizo zinakutana kwa mara nyingine baada ya awali kukutana katika kufuzu robo fainali na Pazi ilishinda pointi 63-50 dhidi ya JKT.

Hata hivyo, JKT inayojivunia nyota wake kama Omary Sadiki, Baraka Sabibi, Jordan David, Jackson Brown na Isakwisa Mwamusope ikiongozwa na kocha Chriss Weba, licha ya kupoteza mchezo huo, ilibadilika katika mechi zilizofuata na kuonyesha ubora hali inayoleta maswali ya nani atakayeibuka mbabe.

Mafanikio ya timu hiyo, yamechangiwa pia na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa, Charles Makene, Frank Kusiga na Frank Simkoko walioonekana wakitoa mawaidha wakiwa nje ya uwanja.

Katika mchezo wao wa nusu fainali, Pazi inatakiwa kumchunga Sadiki anayesifika kwa kumiliki mpira bila ya kupokonywa, pamoja na uwezo wa kufunga na kutoa asisti. 

KIKA 04

UTAMU wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) umedhihirishwa kutokana na kuzidi kukua kwake tofauti na miaka ya nyuma, ikiwamo ongezeko la timu.

Katika ligi ya sasa, jumla ya timu 16 za wanaume zinashiriki sawa na zile za wanawake, kutoka 12 na tisa mtawalia, huku uongozi wa ligi hiyo, Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD) ukizidi kuhamasisha uchezwe na kila mtu.

Kutokana na hamasa hiyo, baadhi ya timu zilifanya usajili mkubwa na kulazimika kuwa na timu mbili zikiwamo kongwe za Vijana ‘City Bulls’, Savio, JKT, na ABC.

Vijana iliunda timu nyingine za Jogoo na Yellow Jacket zilizowahi kushiriki ligi hiyo, huku Savio ikiwa na Magone, JKT (Mgulani JKT), Oilers (Srelio) na ABC (PTW).

Kwa upande wanawake zilizoongezeka ni Kurasini Divas, Mgulani Stars, Twalipo Queens, City Queens, UDSM Queens, Reel Dream na Tausi Royals.

KIKA 01

Ubora wa ligi hiyo umesababisha ongezeko la timu kufikia 25 kutoka 16 zilizoshiriki Ligi Daraja la Kwanza mwaka jana na zilizoongezeka ni Jogoo, KR-one, Yellow Jacket, Christ the King, UDSM Insiders, Polisi DSM, Mbezi Beach Spurs, Dar Kings, Veins BC, Ukonga Kings na Ukonga Warriors.

Zingine ni Oilers, Kigamboni Heroes, Mgulani Heroes, Tz Prisons, DB Magone Kibada Riders, Cavaliers, Kigamboni Academy, Magnets na TRA Sports.

Kamishina wa ufundi na mashindano wa ligi hiyo, Haleluya Kavalambi alisema timu zitakazoshiriki Ligi ya Daraja la Kwanza mwaka huu ni zitakazowahi kulipa ada ya ushiriki.