Mwenyekiti wa CHADEMA Iringa Mjini, Frank Nyalusi Afariki Dunia – Global Publishers



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Iringa Mjini, Frank Nyalusi, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, Ijumaa Septemba 19, 2025, katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa mapema leo na viongozi wa chama hicho, wakieleza kuwa kwa sasa wanasubiri taratibu za kifamilia kabla ya kutangaza rasmi ratiba ya mazishi.

Marehemu Nyalusi aliwahi kujitokeza mwaka 2020 akiwania kuteuliwa kugombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia CHADEMA, ambapo katika kura za maoni aliishia nafasi ya tatu.

Kifo chake kimeacha simanzi kwa familia, ndugu, marafiki pamoja na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wakimtegemea katika safari ya kisiasa ndani ya chama hicho.