Kama kawaida wakali wa ubashiri Tanzania, Meridianbet wanaendelea na harakati zao za kurejesha kwenye jamii ambapo leo hii waliigusa hospitali ya Mwenge kwa kuwapelekea mashine maalumu kwaajili ya kuwekea sabuni na sanitizer lengo likiwa na kuimarisha usafi.
Hatua hii inatokana na dhamira ya kampuni hiyo kushirikiana na taasisi za afya katika kuimarisha mapambano dhidi ya magonjwa yanayohusiana na usafi wa mikono, hususan katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu wengi. Mashine za Kisasa za Sabuni na Sanitizer (Automatic Soap & Sanitizer Dispensers) zilikuwa ni muhimu sana hospitali hapo.
Msaada huu unalenga kuimarisha jitihada za hospitali hiyo katika kudhibiti maambukizi na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wagonjwa na watembeleaji. Uwekaji wa mashine hizi utawezesha wagonjwa, wauguzi na wageni kuosha mikono kwa urahisi na usalama, hatua muhimu katika kudumisha afya bora.
Utajiri wako upo kwenye michezo ya Kasino siku ya leo ingia na ucheze Poker, Keno, Roulette, Aviator, Superheli na ukusanye maokoto zaidi na zaidi. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz kubashiri mechi zote.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Afisa Mahusiano wa Kampuni hiyo Nancy Ingram alisema kuwa, “Katika Meridianbet tunaamini kuwa kusaidia hospitali kwa vifaa vya muhimu kama hivi ni njia ya kuhakikisha usalama wa wagonjwa na wahudumu. Usafi ni kinga ya kwanza dhidi ya magonjwa, na tunajivunia kushirikiana na Hospitali ya Mwenge katika harakati hizi.”
Uongozi wa Hospitali ya Mwenge umeishukuru Meridianbet kwa msaada huu muhimu, na kusisitiza kuwa mashine hizo zitasaidia kwa kiwango kikubwa katika kudumisha viwango vya juu vya usafi hospitalini.
Hii ni sehemu ya mwendelezo wa miradi ya CSR ya Meridianbet, ikidhihirisha dhamira yake ya kuinua jamii kupitia miradi yenye tija, huku ikiendeleza nafasi yake kama kiongozi katika sekta ya michezo ya kubashiri na mshirika wa kweli wa maendeleo ya jamii.
Pia Meridianbet itaendelea siku zote kuwaunga mkono watu wenye uhitaji katika jamii yetu kwani wao na jamii wanategemeana kwa kila kitu. Lakini pia Kampuni hiyo inawashihi watu kutunza mazingira kwa kutokutupa taka hovyo ili kujiepusha na magonjwa mbalimbali.
Leo hii mechi kibao zinaendelea ambapo ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yanapatikana Meridianbet pekee. Ingia na utengeneza jamvi lako la ushindi hapa.