Askofu Novatus Rugambwa Kuagwa Dar, Kuzikwa Bukoba – Global Publishers



Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) imetangaza ratiba ya kuaga na mazishi ya Askofu Mkuu Novatus Rugambwa aliyefariki dunia Septemba 16, 2025 huko Roma, Italia.

TEC imesema Askofu Rugambwa, aliyewahi kuwa Balozi na Baba Mtakatifu huko New Zealand, atakumbukwa kwa utumishi wake wa muda mrefu kwa Kanisa Katoliki na Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Clement Kihiyo, misa ya kumuaga itafanyika Jumamosi, Septemba 27, 2025 saa 3:00 asubuhi katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam. Misa ya mazishi itafanyika Jumatatu, Septemba 29, 2025 saa 3:30 asubuhi katika Kanisa Kuu Jimboni Bukoba.

TEC imewaomba waamini wote waendelee kumuombea Askofu Mkuu Rugambwa na familia yake.

“Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele Umuangazie. Apumzike kwa Amani, Amina,”