MRATIBU KAMPENI ZA CCM ZANZIBAR ATAJA SABABU ZA MSINGI ZINAZOTOSHA DK.SAMIA KUSHINDA KWA KISHINDO

 Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MRATIBU wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Mohamed Abood Mohamed ameeleza hatua kwa hatua sababu za Watanzania kumchagua Mgombea Urais Dk.Samia Suluhu Hassan kuchaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025.

Miongoni kwasababu hizo ambazo zinafanya mgombea huyo wa CCM Dk.Samia kushinda kwa kishindo ni jinsi ambavyo katika minne ya uongozi wake amefanikiwa kuing’arisha Tanzania na Zanzibar sambamba na kuongoza kwa falsafa yake ya umoja na maridhiano ambayo imeifanya nchi imepata utulivu mkubwa.

Akizungumza leo Septemba 20,2025 katika  mkutano wa kampeni za mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, Mohammed amesema Chama hicho kiliamua  kumuomba Dk.Samia na Dk.Hussein Ali Mwinyi ili wawe  wagombea wao kwa  wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kiti cha urais Zanzibar.

“Tunaposema miaka mitano tena tunasema kwa kujua kwa maana yetu kwasababu Dk.Samia umetufanyia mengi mazuri katika uongozi wako wa miaka minne,tumeona maono yako ya kuona mbali”

“Tumeona utu wako, uvumilivu wako na tumeona ulivyo makini katika kufanya maamuzi makubwa ya maendeleo ya nchi yetu.Umeing’arisha Tanzania unaing’arisha Pemba , na ndio maana wananchi  wamejitokeza kwa wingi kuja hapa.

“Umelinda misingi ya uhai wa Taifa na umelinda Mapinduzi na mafanikio yake , umeulinda muungano wetu na umeuimarisha zile tulizokuwa tunaziita kero zimemalizika …

“Lakini kwasababu Muungano ni kitu kinachoishi na kinagusa maisha ya watu zitatokea changamoto ndogo ndogo lakini tunashukuru kwa namna ulivyowezesha kutimiza wajibu wako katika kuimarisha na sasa watanzania wa pande zote mbili wanaishi mahala kokote bila kubughudhiwa wanapofanya shughuli zao za maisha,”amesema.

Ameongeza kwa Dk.Samia jambo kubwa zaidi ni sana  falsafa yake  ya umoja na maridhiano kwani nchi imepata utulivu mkubwa.

“Hata hivyo unavyoona leo hapa wananchi kuwa wengi ni kwasababu wameona namna ulivyosimamia amani na utulivu na matokeo ya amani ya utulivu inawapa nafasi wananchi kufanya shughuli zao za kujitafutia riziki na kujipatia kipato cha kuendesha maisha.Tunakushukuru.

“Katika uongozi wako ukatuunganisha na jumuiya za kimataifa leo watanzania tunaheshima kubwa na kila tunakokwenda duniani wanakuuliza unatoka kwa Samia.

“Kwasababu ya juhudi yako unayoifanya kutuunganisha katika Kimataifa na hukuisha hapo ukabuni filamu ya The Royal Tour.Nikwambie mama kilichotokea Zanzibar utalii umekuwa  na kukua kwa utalii kumewezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kuimarika.

“Jitihada zako tunazifurahia  na Oktoba 29 tutapiga kura kwako Dk.Samia na kwa Dk.Mwinyi .Wapo wenye maneno lakini kekele za mlango hazimkeri mwenye nyumba kulala waache waseme usiku watalala.

“Lakini ikifika Oktoba 29 tutapiga kwako kwa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kura kwa mgombea urais Zanzibar,kura kwa wabunge,Wawakilishi na madiwani.”

Pamoja na hayo amesema CCM inautaratibu wake wa kupata wagombea na wakishapatikana wale waliojitokeza wanaungana.Sasa wenye papara yao ya kuokota wajue walikuwa na  Edward Lowassa (sasa marehemu)wakamkimbilia halafu akarudi nyumbani CCM.

“Tulikuwa naye ndugu yangu Bernard Membe (Mungu amrehemu) wakamkimbilia akarudi nyumbani, sasa nawaambia wasije kulalamika kwa huyo waliokwenda kumfuta kummbatia.”