GCLA YAWAFIKIA WANANCHI MAONESHO YA MADINI GEITA

Meneja wa Usajili na Ukaguzi wa Maabara za Sayansi Jinai na Vinasaba vya Binadamu, Fidelis Segumba (kushoto), akimsikiliza mdau aliyetembelea banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Meneja wa Mamlaka, Ofisi ya Kanda ya Ziwa, John Wanjala (kushoto), akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda la Mamlaka kuhusu majukumu ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Watumishi wa Mamlaka (kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya Mamlaka katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Wananchi na wadau mbalimbali wakisoma majarida na vipeperushi katika banda la Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Watumishi wa Mamlaka (kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu ya Mamlaka katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Wananchi waliotembelea banda la Mamlaka wakisaini na kuandika maoni yao katika kitabu cha wageni baada ya kupata elimu kuhusu majukumu ya Mamlaka katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.

Wadau waliotembelea banda la Mamlaka wakiandika vitu muhimu wakati wakipata elimu kutoka kwa wataalam kutoka Mamlaka kwenye Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.