ETDCO YAENDELEA KUTAFUTA FURSA JAPAN

Uongozi wa Kampuni ya ETDCO, Toyota Tsusho Corporation, Afisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya umeme. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Toyota Tsusho Corporation, jijini Tokyo, Japan.

……………..

Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme (ETDCO) inaendelea kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano na Kampuni mbalimbali nchini Japan.

Kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, ETDCO imepata fursa ya kukutana na Kampuni mbalimbali zikiwemo Toyota Tsusho Corporation na UPDATER INC, kwa lengo la kujadili ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini Tanzania.

Akizungumzia umuhimu wa ushirikiano huo, Kaimu Meneja Mkuu wa ETDCO, CPA. Sadock Mugendi, amesema kuwa hatua hiyo imetoa fursa kwa Kampuni kubadilishana uzoefu, kujitangaza, na kutafuta ushirikiano na makampuni yanayojihusisha na ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umeme nchini Japan.

CPA. Mugendi ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Japan kwa kuratibu mikutano hiyo muhimu.

Makampuni hayo yameonesha nia ya kushirikiana na ETDCO kwa kuangalia namna bora ya kushirikiana katika Sekta ya ujenzi na Ukarabati wa miundombinu ya umeme.