Jasinta Makwabe Atoa Kauli Nzito Kuhusu Diamond Platnumz – Global Publishers



Mwanamitindo maarufu wa Afrika Mashariki, Jasinta Makwabe ‘Candy Boo’, amewasha moto mitandao baada ya kudaiwa kutoa kauli nzito inayozua mjadala mkubwa. Amesema staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, hana nafasi ya kumkwepa endapo akiamua kumvutia.

Candy Boo amesema wazi: endapo atataka kupata mtoto na Diamond, jambo hilo linaweza kutimia mara moja bila kikwazo chochote.

“Hakuna mwanaume asiyevutiwa kimapenzi na mimi, hata huyo Diamond Platnumz nikimwambia nataka mtoto, hawezi kuchomoa kabisa. Kuna kipindi aliniambia anatamani kupata mtoto na mimi, ila sikuwa tayari kwa hilo,” amesema Jasinta.

Kauli hii imeibua mijadala mikali mitandaoni; baadhi ya mashabiki wakimtaja Candy Boo kama “malkia wa mvuto”, huku wengine wakiona ni mbinu ya kutafuta kiki kupitia jina la Diamond.