Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa elimu maalum kwa wafanyabiashara baina ya Tanzania na Afrika Kusini kuhusu masoko ya fedha za kigeni sambamba na muelekeo wa hali ya kiuchumi hususani nchini Tanzania. Hatua hiyo ililenga kuwajengea uwezo na ufanisi zaidi wafanyabiashara hao utakaowasaidia kufanya uamuzi sahihi kwenye masuala yanayohusu manunuzi ya fedha hizo na uwekezaji.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Idara Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki ya NBC Bi Juliana Mwapachu ambae alipata wasaa wa kuwasilisha mada kuhusu hali ya masoko ya fedha za kigeni nchini alisema, uelewa zaidi kuhusu masoko ya fedha za kigeni kwa kiasi kikubwa utawaepushia hasara kubwa wanayoipata wafanyabiashara hao pindi wanapofanya manunuzi ya fedha hizo bila kuzingatia vigezo tofauti vya kiuchumi.
“Huu ni mwendelezo tu wa jitihada zetu kama benki kinara katika kuwahudumia wafanyabiashara baina ya mataifa haya mawili ambapo tumekuwa tukiwasilisha mada tofauti za kiuchumi na biasahara ili kuwajengea uelewa zaidi kuhusu uendeshaji wa biashara zao kwa namna ambayo ni rafiki zaidi kwa taasisi za kifedha na mamlaka tofauti ili wasijukute kwenye changamoto ambazo zinaweza kuwakwamisha kibiashara zao,’’ alisema.
Akiwasilisha mada hiyo mbele ya wanachama wa jukwaa hilo Bi Mwapachu alielezea kwa upana kuhusu hali ya kiuchumi wa Tanzania kwa mwaka 2025 huku akielezea matarajio na muelekeo wa wa hali ya kiuchumi kwa mwaka ujao 2026.
“Kupitia uelewa wa kutosha kuhusu hali ya masoko ya fedha za kigeni tunaamini wafanyabiashara hawa watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanya uamuzi sahihi kuhusu ni wakati gani na namna gani sahihi zaidi kwa wao kununua na kubadili fedha za kigeni kwa viwango rafiki ambayo vitawaepushia wao kupata hasara zitokazo na tofauti ya thamani ya fedha hizi kwenye masoko ya fedha za nje.’’ Alisema.
Alisema mbali na huduma za fedha za kigeni benki hiyo imejipanga zaidi kuendelea kuwahudumia wafanyabiashara hao kwenye maeneo mengine zaidi ikiwemo ushauri wa kitaalum pindi wanapohitaji kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania likiwemo nchi ya Afrika Kusini.
Mbali na wanachama wa jukwaa hilo mkutano huo pia ulihusisha wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali, maofisa wa ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania pamoja na maofisa kutoka benki ya NBC ambayo ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa mkutano huo.
Akizungumzia umuhimu wa elimu hiyo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Bw Manish Thakrar alisema kwa kiasi kikubwa itawasaidia wafanyabiashara hao ambao wamekuwa wakifanya manunuzi ya fedha mbalimbali za kigeni pindi wanapohitaji kuagiza mizigo ya biashara mbalimbali kutoka nje ya nchi.
“Elimu hii ina msaada mkubwa sana kwa sisi wafanyabiashara hasa kipindi hiki ambacho bei ya thamani Dola ya Kimarekani imeshuka kwa karibu sh 200 ya kitanzania.Kupitia elimu hii sasa wafanyabiashara wataelewa kuwa huu ni wakati sahihi zaidi kwa wao kuagiza na kutoa bidhaa nje ya nchi hatua ambayo itachochea zaidi ufanyikaji wa biashara na kukuza Uchumi wetu zaidi.’’ Alisema.
Zaidi Bw Thakrar alitoa wito kwa serikali ihakikishe inaendelea kusimamia na kuongoza mikakati thabiti itayosaidia kuimarisha uimara wa thamani ya shilingi dhidi ya fedha tofauti za kigeni hususani Dola ya Kimarekani hatia ambayo itasaidia kuendelea kukuza ustawi wa biashara nchini pamoja na kupunguza mlipuko wa bei hususani kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Mkuu wa Idara Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki ya NBC Bi Juliana Mwapachu (alieshika mic) akiwasilisha mada maalum kuhusu hali ya masoko ya fedha za kigeni nchini wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Hatua hiyo ililenga kuwajengea uwezo na ufanisi zaidi wafanyabiashara hao utakaowasaidia kufanya uamuzi sahihi kwenye masuala yanayohusu manunuzi ya fedha hizo na uwekezaji. Benki ya NBC ilikuwa mdhamini mkuu wa mkutano wa jukwaa hilo.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania, Bw Manish Thakrar (alieshika) akizungumza na wanachama wa jukwaa hilo wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Idara Masoko ya Fedha za Kigeni wa benki ya NBC Bi Juliana Mwapachu (alieshika mic) akijadili mada maalum kuhusu hali ya masoko ya fedha za kigeni nchini wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABF) uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Hatua hiyo ililenga kuwajengea uwezo na ufanisi zaidi wafanyabiashara hao utakaowasaidia kufanya uamuzi sahihi kwenye masuala yanayohusu manunuzi ya fedha hizo na uwekezaji. Benki ya NBC ilikuwa mdhamini mkuu wa mkutano wa jukwaa hilo.
Mbali na wanachama wa jukwaa hilo mkutano huo pia ulihusisha wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali, maofisa wa ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania pamoja na maofisa kutoka benki ya NBC ambayo ndio ilikuwa mdhamini mkuu wa mkutano huo.
Baadhi ya washikiri wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania wakichangia mada wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Washikiri wa Mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania walipata wasaa wa kubadilishana mawazo wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.