Kwa msaada wa polisi wa usalama barabarani pikipiki ilikamatwa mara moja. Ilikutwa katika kituo cha bodaboda cha Kwaminchi. Mwenye pikipiki ndiye huyu hapa niliyekuja naye. Sasa nataka na yeye mumsikilize.” Inspekta Amour akamatazama yule kijana wa bodaboda.
Bado Watatu – 38
