Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Meneja wa Kanda Kati wa Mamlaka ya Uwekezaji Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Bwana Venance Mashiba amesema kuwa Serikali kupitia Mamlaka hiyo imekuja kuhamasisha Uwekezaji wa Ujenzi wa Viwanda katika eneo linalomilikiwa na TISEZA lililopo katika eneo la Viwanda Nala Jijini Dodoma kwa kutoa eneo bure kwa Mwekezaji atakayekuwa na sifa zilizotolewa na Mamlaka hiyo.
Ambapo ameainisha sifa ambazo anapaswa kuwa nazo mwekezaji kuwa ni, mwekezaji wa ndani ni awe na uwekezaji wenye thamani isiyopungua Dola Milioni 5 lakini kwa mwekezaji wa nje kuwa na uwekezaji wenye thamani isiyopungua Dola Milioni 10 sambamba na kuweza kutengeneza Ajiara zisizopungua 1,000 za moja kwa moja na zingine zisizo za moja kwa moja.
Mashiba ameyeeleza hayo leo hii Jijini Dodoma Septemba 23,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika eneo Maalum la Uwekezaji lililopo Nala Jijini Dodoma ambalo linamilimiwa na Mamlaka hiyo.
“Tunawaita walio tayari waje,Serikali imeamua kuhamasisha kwa kulitoa eneo hili bure kwa mwekezaji yeyote ambaye atakuwa na sifa ambazo zimetolewa na Mamlaka”.
“Sifa zenyewe zilitolewa na Mamlaka ni kwamba kama mwekezaji wa ndani basi awe na tayari uwekezaji wenye thamani isiyopungua Dola Milioni 5,lakini kama ni mwekezaji wa nje basi uwekezaji wake uwe na thank isiyopungua Dola Milioni 10”.
Aidha amesema kuwa muitiko wa Kampeni hii ni mkubwa kwani tangu walipozindua kampeni hii hapo Agosti 12,2025 mpaka sasa wana Maombi ya Wawekezaji wa nne ambao wako tayari kuanza kufanya uwekezaji katika eneo hilo ambapo hao wakiwa ni Wawekezaji wa ndani.
Kwa upande wake Pendo Gondwe ambaye ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano TISEZA ameeleza kuwa mbali na Serikali kutoa fursa ya kutoa eneo bure kwa Mwekezaji atakayekuwa na Nia ya kuwekeza na kuahidi kujenga kiwanda ndani ya mwaka mmoja bila kuwepo kwa gharama zozote, lakini pia bado Serikali hiyo imeondoa mapunguzo mbalimbali ikiwemo kodi kwenye uingizaji wa Mitambo,uingizaji wa malighafi pamoja na kuondoa kodi kabisa katika baadhi ya maeneo.