ONYESHO LA KIHISTORIA LA KUDANSI KUFANYIKA MAKUMBUSHO

Vijana wa Dar es
salaam Dances International (DDI) wakifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi onyesho
la kihistoria la kudansi lilotarajiwa kufanyika Katika Ukumbi wa Maonesho wa
Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam (picha na Mussa Khalid)

…………….

NA MUSSA KHALID

Tamasha la Museum Arts
Explosion
 kwa kushirkiana na Dar es salaam Dances
International (DDI) wameandaa onyesho Maalum la Kihistoria na kiutamaduni la kudansi
linalotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Sept 26 mwaka huu.

‎Akizungumza
jijini Dar es salaam wakati wa mazoezi ya kujiandaa kuelekea siku hiyo Kiongozi
na Mwaasisi wa Kundi hilo Abdulkarim Juma maarufu Tayzdullah amewaomba
watanzania kushiriki kwa wingi katika Maonesho hayo ili kuona Vijana wa
kitanzania wakionyesha uwezo wao.

‎Aidha
amewasisitiza Vijana kuepuka kukaa vijiweni badala yake watumie fursa ya
kutumia vipaji vyao jambo litakalosaidia waweze kujikwamua kiuchumi na
kuitangaza vyema Tanzania

“Tunawaomba
wadau mbalimbali kushiriki siku hiyo kwani uwepo wao ni muhimu sana kwetu sisi
kwa kjutuonyesha ushirikiano katika onyesho tunalolifanya’amesema Tayzdullah

‎Naye
Choga Choga maarufu Dallazy amesema watu watakapojitokeza watashuhudia onyesho
la kihistoria kwani wamekuwa wakifanya katika maeneo mbalimbali nchini na nje
ya nchi.

Amewasisitiza
wananchi kujitokeza kwa wingi ili waweze kujionea na kujifunza utamaduni kutoka
kwa vijana hao katika onyesho lao watakalolifanya kwani litakuwa ni tukio kubwa
la kisanaa.

Tamasha la Dar es
Salaam Dances International, lililohuishwa na maonyesho ya kusisimua,na sanaa
ya kustaajabisha wanashiriki  wasanii
mahiri kutoka pande mbalimbali ambapo hilo ni zaidi ya tukio la sherehe ya
sanaa, utamaduni, na uvumbuzi
 lilotarajiwa
kufanyika Katika Ukumbi wa Maonesho wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es
salaam.