MAKINIKIA TANZIA: KAPTENI ABBAS MWINYI KUZIKWA KESHO UNGUJA, RAIS MWINYI ASITISHA ZIARA YAKE YA KAMPENI KISIWANI PEMBA

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia CCM, amewasili Unguja akitokea Pemba kufuatia msiba mzito wa kaka yake, Mhe. Kapteni Abbas Ali Mwinyi, aliyefariki dunia leo tarehe 25 Septemba 2025 katika Hospitali ya Lumumba, Unguja.

Marehemu Kapteni Abbas, ambaye pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Fuoni na rubani wa ndege wa muda mrefu kabla ya kustaafu na kujitosa kwenye siasa, atazikwa kesho tarehe 26 Septemba 2025 nyumbani kwao Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja, mara baada ya Sala ya Ijumaa.