Pamoja na pongezi hizo,
Jenerali Mkunda amempandisha cheo kutoka Sajini kuwa Sajinitaji tukio lililofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi Upanga Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Septemba 2025.
Amesema ushindi huu ni kwa watanzania wote na Afrika kwa ujumla na kwamba michezo ni sehemu ya kazi jeshini hivyo Sajinitaji Alphonce Simbu amefanya kazi nzuri.
Jenerali Mkunda ametoa rai kwa Maafisa na Askari wote jeshini waige mfano wa Sajinitaji Simbu kwa kufanya kazi kwa bidii na kuleta mafanikio katika kila idara jeshini.

Naye, Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema safari hii katika michezo Jeshi limefanya vizuri sana ambapo tarehe 26 Septemba 2025 Katika Uwanja wa Golf Lugalo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi atapokea vikombe kutoka timu za Jeshi zilizofanya vizuri katika Mashindano

Related