Mrembo maarufu na msanii wa mitindo nchini Tanzania, Surraiya Rimoy maarufu kama Sanchi (@surraiyaworld), anadaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rajab Abdul Kahali ‘Harmonize’.
Tetesi hizo zimechochewa zaidi baada ya kusambaa kwa video mtandaoni ikionyesha wawili hao wakiwa pamoja katika mazingira ya karibu, hali iliyowafanya mashabiki kuanza kubashiri kwamba huenda kuna kitu zaidi ya urafiki.
Baadhi ya mashabiki wametoa maoni tofauti kwenye kurasa za mitandao ya kijamii. Wapo waliopongeza hatua hiyo wakisema “wanapendeza pamoja”, huku wengine wakiona ni dalili ya mapenzi mapya ya Harmonize, ambaye mara kadhaa ameweka wazi kutamani uhusiano wa kudumu.
Sanchi amekuwa miongoni mwa wanamitindo maarufu zaidi nchini, mwenye mashabiki wengi mitandaoni na mara kwa mara akihusishwa na tetesi za mahusiano na mastaa. Video hiyo imeongeza moto kwenye jina lake, hasa kutokana na ukaribu wake na Harmonize.
Hata hivyo, mpaka sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Harmonize wala Sanchi kuhusu madai ya kuwa katika mahusiano. Wawili hao wameendelea na shughuli zao kama kawaida, huku mashabiki wakisubiri kuona kama tetesi hizi zitathibitishwa au kukanushwa.
Related