Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe ametoa ahadi nzito kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika, akisema kama Yanga isiposhinda kwa kishindo atakubali kupigwa makofi.
Akizungumza klabuni hapo, Kamwe amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo wenye wasiwasi na timu yao akisema mfumo uwanjani umeshakubali.
Kamwe amesema wameshajaribu kila kitu kuelekea mchezo huo wa marudiano dhidi ya Wiliete na kwamba, mammbo yakuwa mazuri na watashusha mziki mzito.
“Tumekuja na kaulimbiu kwamba mfumo umekubali. Tumeshajaribu vitu, tumeona vimekubali. Kesho tutakwenda kufungulia busta zetu,” amesema Kamwe.
“Nina uhakika asilimia mia moja msipoona mafuriko kesho pangeni foleni hapo wote na wanaonisikia kila mmoja anipige makofi. Mimi sidanganyi kwa kuwa naujua mpira.”
Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kufika kwa wingi uwanjani ili kuwaunga mkono wachezaji wao kwa kuwa mpaka sasa timu hiyo imeshinda mechi zote kuanzia za kirafiki mpaka mashindano.