Simba, Yanga kuna kazi Oktoba 9

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa ratiba ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) itakayoanza kuchezwa kwa mechi za nusu fainali ya Ngao ya Jamii zitakazopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.

Timu zilizomaliza nafasi nne katika msimamo wa Ligi ya msimu uliopita ambazo ni bingwa mtetezi JKT Queens, Simba Queens, Yanga Princess na JKT Queens.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na TFF, Simba iliyomaliza nafasi ya pili itakutana na Mashujaa, huku bingwa wa Ligi, JKT itaumana na Yanga Princess  wakati fainali ikitarajiwa kupigwa Oktoba 12.

Hii ni mara ya tatu tangu michuano hiyo ifanyike mwaka 2023 ambapo Simba Queens ilitwaa taji hilo baada ya kuitandika JKT Queens kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1.

Mwaka jana JKT ikawapokonya Wekundu wa Msimbazi taji hilo baada ya kuitandika Yanga Princess bao 1-0 katika fainali iliyochezwa KMC Complex.