Wajumbe UN walivyosusia hotuba ya Netanyahu, wengine wazomea

New York. Wajumbe wengi wa mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamesusa kwa kutoka nje ya ukumbi wakati Waziri Mkuu wa Israel, wakati Benjamin Netanyahu alipoanza kutoa hotuba yake aliyoitoa leo Ijumaa Septemba 26, 2025.

Wakati Netanyahu alipoanza kuhutubia, watu wengi ndani ya ukumbi walianza kumzomea na kuondoka ukumbini ikiwa ni ishara ya kupinga yanayoendelea Gaza, huku wengine wakimpigia makofi.

Wakati hayo yakiendelea mwenyekiti wa mkutano huo alianza kuwatuliza ikiwa ni kutaka utulivu ndani ya ukumbi na kumpa nafasi mzungumzaji huku akisema “Tafadhali, utulivu ukumbini.”

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa alisema mapema kuwa alikuwa anafahamu kuhusu tukio hilo la kususa, akidai kuwa lilipangwa na ujumbe wa Palestina nchini Marekani. Tukio kama hilo lilitokea pia mwaka 2024.

Hotuba ya Netanyahu yake inakuja baada ya mataifa kadhaa ya Ulaya, yakiwemo Uingereza, kutangaza rasmi kutambua taifa la Palestina.

Wajumbe walitoka kwa hasira muda mfupi kabla ya Netanyahu kuanza hotuba yake katika mkutano wa Umoja wa Mataifa, huku Netanyahu mwenyewe akitangaza kuwa kutambuliwa kwa Palestina na mataifa ya Magharibi kunaonesha kuwa ‘kuwaua Wayahudi kunalipa’.”

Kuonyesha kwamba hawafurahishwi na kinachoendelea Gaza wajumbe kutoka sehemu mbalimbali za dunia walitoka kwa katika ukumbi wa mkutano wakati Netanyahu alipokuwa akijiandaa kutoa hotuba yake ya kutetea vita vya Israel huko Gaza.

Hata hivyo, Netanyahu aliendelea na hotuba yake akiwashambulia viongozi wa nchi za Magharibi akisema; “wanaokatishwa tamaa mbele ya uovu, hamtaepuka dhoruba ya jihadi kwa kumtupa Israel.

“Hapa kuna ujumbe mwingine kwa viongozi wa Magharibi: Israel haitawaruhusu mnajaribu kulazimisha kutoa taifa la kigaidi mdomoni mwetu.

“Hatuwezi kujiua kitaifa kwa sababu hamna ujasiri wa kukabiliana na vyombo vya habari vinavyotishia na umati wenye chuki dhidi ya Wayahudi unaodai damu ya Israel.”

Akimlenga Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer na viongozi wengine wa dunia, Netanyahu aliongeza: “Uamuzi wenu wa aibu utaongeza ugaidi dhidi ya Wayahudi na dhidi ya watu wasio na hatia kila mahali.

“Hamas hufundisha watoto kuwapinga Wayahudi na kuharibu taifa la Wayahudi… Hawa ndio watu mnataka kuwapa taifa? Mninachokifanya ni kuwapa zawadi ya juu zaidi wafuasi waharakati waliotekeleza na kuunga mkono mauaji ya Oktoba 7, 2023.

“Kuwapa Wapalestina taifa maili moja kutoka Jerusalemu baada ya Oktoba 7,2023 ni kama kuwapa Al-Qaeda taifa maili moja kutoka New York City baada ya Septemba 11. Hii ni wazimu kabisa. Ni kichaa, na hatutafanya hivyo.”

Katika hotuba yake, Netanyahu aliwajibu moja kwa moja Wapalestina walioko Gaza akisema vita vinaweza kumalizika mara moja kwa kurudishwa kwa mateka, kuwapokonya silaha Hamas, na kuondolewa kwa silaha kutoka Ukanda wa Ghaza.

Kama ambavyo amekuwa akifanya hapo awali, katika hotuba yake, Netanyahu alinyanyua kifaa cha kuonesha picha na ramani ya eneo hilo yenye kichwa ‘LAANA’, kabla ya kuichora kwa alama kubwa kwa kutumia kalamu.

Katika hatua ya kushangaza, Netanyahu pia alifichua kuwa hotuba yake ilikuwa inatangazwa moja kwa moja ndani ya Gaza kupitia vipaza sauti vikubwa vilivyowekwa mpakani na Israel.

Ofisi ya Netanyahu inadai kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limechukua udhibiti wa simu za raia wa Kipalestina na wapiganaji wa Hamas walioko Gaza, na hotuba yake hiyo katika Umoja wa Mataifa sasa inatangazwa moja kwa moja kupitia vifaa hivyo.

Inaripotiwa kuwa wakazi wa Gaza walipokea ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wenye kiungo cha hotuba ya Netanyahu, ingawa hakuna uthibitisho wa haraka kuwa vifaa hivyo vilichukuliwa na kudhibitiwa.

Hotuba ya Ijumaa ilikuwa nafasi yake ya kujibu jumuiya ya kimataifa kwenye jukwaa lake kuu zaidi.

Alisema kwamba Israel imeharibu sehemu kubwa ya “mashine ya ugaidi” ya Hamas, na inalenga kukamilisha kazi hiyo “haraka iwezekanavyo.”

Netanyahu alisherehekea kile alichokiita ushindi wa kimkakati wa Israel katika kipindi cha mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na kulenga mpango wa nyuklia wa Iran na kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, nchini Lebanon.

Imeandikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao