::::::::::
Viongozi mbalimbali wa Tanzania wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango wameshiriki mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) New York.
Pia, Mtanzania Balozi Liberata Mulamula ambaye ni Mjumbe Maalum Umoja wa Afrika, kuhusu Agenda ya Wanawake, Amani na Usalama, ameshiriki mkutano huo.
Viongozi wengine walioshirki huo ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo, Kaimu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (UN).
Dk.Mpango ameshiriki mkutano huo na kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa akimwakilisha Mhe. Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo ameambatana na Mke wake Mama Mbonimpaye Mpango.
Pamoja na Mambo mengine Dk.Mpango ameshiriki mazungumzo na viongozi wa mataifa mbalimbali nje ya mkutano huo.
00000
NEW YORK