WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Septemba 28, ameshiriki katika mbio za hisani za Saifee Marathon zilizoanzia na kuishia katika viwanja vya green park Oysterbay, jijini Dar es Salaam.
Lengo la marathon hizo ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kwa kutoa elimu ya afya kwa wananchi kuhusu mtindo bora wa maisha.
Lengo lingine ni kuimarisha uchunguzi wa mapema wa magonjwa yasiyoambukiza, pamoja na kuhimiza ushirikiano wa wadau mbalimbali katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza.