AICC KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZAKE

Na Mwandishi wetu

KITUO cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC)kimesema kuwa kinaendelea kuboresha kumbi zake mbalimbali huku kikiwakaribisha wadau wa kimataifa na kitaifa kufanya shughuli zao za mikutano katika kumbi zao kutokana na madhari uwepo wa madhari nzuri.

Akizungumza leo Septemba 26,2025 wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonesho ya 22 ya wahandisi yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mlimani City,Ofisa Mawasilino na Uhusiano,Mourine Kaaya amesema katika kuendesha mikutano mbalimbali katika kumbi zao ikiwemo Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) imekuwa mstari wa mbele katika kutoa mchango wake mkubwa wa kuongeza pato la taifa.

Amesema licha ya wao kufaidika lakini na wananchi wanaoishi katika mikoa ya Dar es Salaam na Arusha wamekuwa wakinufaika na uwepo wa kumbi hizo kutokana na kuwaongezea kipato.

“AICC imekuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa,pia kwa wananchi mmoja mmoja kutokana na wageni wanaokuja kwenye kumbi hizi na kufanya mikutano uhitaji sehemu za kulala,Usafiri na Chakula wakati mwingine.

“Hii ni hatua kubwa kwa AICC katika kupata mafanikio yake na sio kwa AICC tu bali kwa taifa kwa ujumla katika kuongezea Pato la nchi,”amesema Kaaya.

Kaaya amesisitiza kuwa kumbi ya AICC hina kumbi za mikutano pekee bali zina kumbi nyingine ndogo ndogo za kawaida kwaajili ya Sherehe mbali mbali kama harusi na hafla nyingine.

“Tunawakaribisha wadau wote kwa huduma za kukodi kumbi zetu kwani hatujihusishi na mikutano ya kimataifa tu bali tunajumuisha na mikutano ya ndani ya kawaida,”amesisitiza