::::::
NA. MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Chakula na Lishe Dkt. Germana Leyna ametoa wito kwa wadu wa masuala ya lishe nchini kuendelea kuunga mkono jitihada za kupambana na changamoto zinazokabili masuala ya Lishe huku akisema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabili changamoto hizo kwa kuwa na mikakati madhubuti.
Wito huo umetolewa leo 29 Septemba, 2025 kwenye mahojiano maalumu katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jijini Dar es Salaam katika kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa 11 wa Wadau wa Masuala ya Lishe.
“Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimabli ikiwemo kuendelea kutoa elimu kwa umma na kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa wa masuala ya lishe ili kuendelea kuwa na Taifa lenye watu wenye lishe bora na niseme apa kuwa wadau waje tunganishe nguvu katika kupambana na changamoto za maswala ya Lishe” amesema Dkt Germana Leyna.
Pia ameongoza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inawafikia wazalishaji hasa wakulima wawapo katika shughuli zao za kilimo na kuhakikisha wanapata elimu ya lishe bora na umuhimu wa kutunza chakula cha matumizi ya nyumbani badala ya kuuza chote.
Ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wadau kuendelea kujitokeza na kuendelea kuweka chachu katika masuala ya lishe nchini.
=MWISHO=