Moto wateketeza bweni la shule ya Wasichana Asha-Rose Migiro

Mwanga. Moto ambao chanzo chake hakija-julikana umeteketeza bweni la Shule ya Wasichana ya Asha-Rose Migiro, linalotumiwa na wanafunzi 347 katika Kitongoji cha Ma-kuyuni, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro.

Mbali na kuteketea kwa bweni hilo, wanafunzi 46 wamepata mshituko na kupelekwa Kituo cha Afya Mwilange kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, Ju-matatu Septemba 29, 2025, na hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza.

Amesema mali zilizokuwemo ndani, ikiwemo vitanda, magodoro na makabati ya nguo, vyote vimeteketea kwa moto.

“Chanzo cha moto huu bado hakijafahamika. Uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini chanzo chake. Hakuna majeruhi, wapo wana-funzi 46 waliopata mshituko wakati tukio linato-kea na walichukuliwa na kukimbizwa katika kit-uo cha afya kwa matibabu zaidi.

 “Katika ajali hii ya moto, bweni moja ndilo lime-teketea kwa moto, lenye vitanda pamoja na magodoro yake 354, makabati ya nguo 32 na shelfu za kuwekea viatu 32,” amesema.

Aidha, amesema jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchukua tahadhari ya kinga dhidi ya majanga ya moto.