AMEIR HASSAN AMEIR: Atamba kumlipa kila Mzanzibari Sh500,000 kwa mwezi akiwa Rais

Dar es Salaam. Chama cha Makini au kwa kifupi Makini, ni matokeo ya kubadilishwa jina kwa Chama cha Demokrasia Makini.

 Bila shaka ni mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya, wala si mvinyo mpya ndani ya chupa ya zamani.

Agosti 25, 2024, Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama hicho, uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Nefaland, Manzese, Dar es Salaam, kwa kauli moja, ulibadili jina la taasisi kutoka Demokrasia Makini hadi Chama cha Makini. Yalikuwa mabadiliko yenye shabaha ya kuchaji nishati kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Makini wapo makini kwenye uchaguzi mkuu 2025. Kuanzia urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, urais wa Zanzibar, ubunge, ujumbe wa Baraza la Wawakilishi mpaka udiwani.

Upande wa urais wa Zanzibar na uenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makini kete yao ni Ameir Hassan Ameir, ambaye ni naibu katibu mkuu wa chama hicho.

Ameir, mwalimu kitaaluma, anaingia kwenye uchaguzi akisema hana hofu. Anawashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa chama chake kwa kumchagua kwa imani kubwa ili akapeperushe bendera ya chama kwenye nafasi ya urais wa Zanzibar mwaka huu.

Ahadi ya Ameir ni kufanya kampeni za kistaarabu ili Wazanzibari wazielewe se-ra zake, vilevile wapate nafasi ya kuchanganua na sera za wengine, kisha wawe kwenye wakati mzuri wa kufanya uchaguzi kwa kutanguliza zaidi kesho ya Zanzibar na nchi nzima ya Tanzania.

Ameir anasema kuwa, anajivunia sera za chama chake, kwa hiyo ana uhakika ku-wa atazitumia vema kujiuza kwenye uchaguzi.

Pia, haoni shida kuwafikia wananchi na kuzungumza nao ili wamwelewe, kwa kuwa sera za Makini ni bora kuliko za vyama vingine vyote.

Anatamba kuwa, ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais wa Sita wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Serikali ilizitumia sana sera za Makini, ndiyo maana ameweza kujenga vituo vingi vya afya na vifaa tiba.

Ameir anasema kuwa sera ya Makini ku-husu afya ni kuwa, “ukimnyima mwananchi huduma za afya ni sawa na kumkosesha haki ya kuishi.”

Kingine, Ameir anasema kwa miaka mi-tano ya muhula mmoja wa Rais wa Zan-zibar na Mwenyekiti wa Baraza la Map-induzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, amekuwa akitekeleza sera za Makini.

Kwa hoja hiyo, anasema itakuwa ni fursa kwa Wazanzibari kumchagua mtu anayetokea kwenye chama chenye sera nzuri.

Kuhusu jinsi anavyouelekea uchaguzi, Ameir anasema atafanya kampeni nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu, kuhakikisha anawafikia wapigakura kwa ukaribu zaidi.

Anasema popote pale atakapoona watu, atasimama kuzungumza nao kisha ataa-cha wamuulize zaidi maswali, kuliko yeye kujieleza.

Yupo mtu akitangaza kuwa anatafuta uongozi ili afanye mapinduzi ya kielimu ni rahisi kumwelewa.

Ameir alipambana sana kuitafuta elimu, kisha akawa mwalimu, na akaitumia taaluma yake kuanzisha shule, yeye aki-wa mwalimu wa kwanza na wa pekee.

 Leo, shule yake imekuwa taasisi, ina walimu 22, wanafunzi 415 na wafan-yakazi wawili wa usafi.

Shule inaitwa Sky View, ipo Melinne Ta-veta, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Ameir alianzisha shule hiyo kama darasa tu la kufundisha kozi ya Kiingereza.

Mwaka 2011, aliamua kuligeuza darasa hilo kuwa shule ya chekechea, ikapanda kuwa shule ya msingi na sasa inasomesha mpaka sekondari.

Kwa sasa Ameir sio tena mwalimu, bali pia mkurugenzi mtendaji wa shule ya Sky View.

Shule inayotoa msaada wa kusomesha bure watoto yatima na wanaioshi kwenye mazingira magumu. Kwa idadi ya sasa, Sky View ina watoto yatima 22 wanaonufaika na elimu bure.

Ameir ni mwenye fomu ya kugombea urais wa Zanzibar mwaka huu, kupitia Chama cha Makini.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ili-shampitisha na kumteua kuwa mgombea urais Zanzibar. Na sasa yupo kwenye kampeni, akiwaangukia Wazanzibari wamwelewe na wamchague awaon-goze.

Kwanza Ameir ni mzaliwa wa Unguja. Alizaliwa Machi 19, 1973, Hospitali ya Mnazi Mmoja, iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi. Nyumbani kwao ambako ndipo alilelewa ni Kwa-Alamsha, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini.

Ameir ni mtoto wa kwanza katika wato-to 21 wa mzee Hassan Ameir Simai, am-baye asili yake ni Paje, Mkoa wa Kusini, Unguja.

 Hata hivyo, Ameir kwa mama yake, Asia Suleiman Mohamed, walizaliwa wawili tu. Asia (mama wa Ameir) ni mzaliwa wa Wambaa, Wilaya ya Kusini, Pemba.

Elimu ya msingi, Ameir alisoma Shule ya Mwanakwerekwe C, Mjini Magharibi B. Alianza darasa la kwanza mwaka 1980 na alimaliza madarasa yote saba katika shule hiyo, kabla ya kuhitimu mwaka 1986.

Ameir baada ya kumaliza shule ya msingi na kwa sababu wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumsomesha, alianza kufanya kazi katika ajira tofauti, hasa za hoteli.

Alihama kwenye ajira ya hoteli moja hadi nyingine; kutoka Blue Bay iliyopo Kiwengwa, Mkoa wa Kaskazini, Unguja mpaka Ocean Paradise, Pwani Mchangani, Mkoa wa Kaskazini.

 Alifanya pia Lagema Del East, Nungwi, Mkoa wa Kaskazini, kisha Bahari Beach, Kunduchi, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ameir, alifanya kazi kama mtumishi wa idara mbalimbali kwenye hoteli hizo, ikiwamo udereva. Baadaye aliona kinachomkwamisha ku-pata mshahara mzuri ni elimu, hivyo pamoja na utu uzima, aliamua kurudi shule na kusoma elimu ya sekondari.

Mwaka 2002, alianza masomo ya sek-ondari kwenye Shule ya Sufa, iliyopo Tomondo, Wilaya ya Mjini, Magharibi B.

 Mwaka 2005, alihitimu kidato cha nne. Mwaka 2006, kwa kujisomesha, alifanya mtihani wa kidato cha sita kama mtahi-niwa binafsi.

Mwaka 2006 baada ya kuwa na cheti cha kidato cha nne, alianza kusoma stahahada ya ualimu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

Hivyo, mwaka 2006, Ameir alipokuwa anapambana kufanya mtihani wa kidato cha sita kama mtahiniwa binafsi, alikuwa pia anasoma stashahada ya ualimu.

Mwaka 2008 alihitimu stashahada ya ualimu, mwaka 2009, alijiunga Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), alikosoma stashahada ya utawala wa biashara. Mwaka mmoja alisoma masomo ya maandalizi ya shahada ya kwanza ya ulinzi wa haki za watoto kwa mwaka mmoja, alipoona gharama za kujisomesha ni kubwa ndipo alianzisha shule.

Wakati wa kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, Ameir alikuwa kada wa CCM na alishiri-ki harakati mbalimbali za kujenga chama akiwa Tawi la CCM Nyerere, lililopo Kwa Ali Mzee, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini. Mwaka 1998, alivutiwa kujiunga na Chama cha UMD, ali-koteuliwa kuwa naibu mshika fedha wa Zanzibar.

Mwaka 1999, Ameir alishirikiana na mwasisi wa Demokrasia Makini, hayati Profesa Leonard Shao, kutambulisha chama hicho Zanzibar.

Na baada ya chama kupata usajili wa kudumu mwaka 2000, Ameir alichagu-liwa na mkutano mkuu kuwa naibu kat-ibu mkuu Zanzibar.

 Mwaka 2010, Ameir alichaguliwa kuwa katibu mkuu. Nafasi anayoishikilia mpa-ka sasa.

Ameir amewahi kugombea ubunge mwaka 2000 na 2005, Jimbo la Fuoni, Mjini Magharibi, kwa tiketi ya Demo-krasia Makini.

Mwaka 2010 na 2015, aligombea ub-unge Jimbo la Pangawe, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi. Mara zote hakuweza kushinda.

Huyo ndiye Ameir wa Makini. Chama kimeshampa leseni ya kupigania urais wa Zanzibar, naye anasema yupo tayari kimwili na kiafya.

Zaidi, anasisitiza kuwa anautaka urais wa Zanzibar 2025 ili aongoze muhula ujao wa Serikali kwa sababu anaona yeye ndiye anaweza kuifanya hiyo kazi kwa ustadi wa hali ya juu.

Anasema kupitia taaluma yake ya ualimu na kwa vile ameishi maisha ya chini kabisa kama Wazanzibari wengi, hakuna kitu ambacho hakijui kuhusu shida za wananchi wa Zanzibar, kwa hiyo anaamini ni yeye tu ndiye anaweza ku-wapa maendeleo Wazanzibari, ambayo hawajawahi kuyapata tangu Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Ameir anasema akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, kisha akaapishwa, siku ita-kayofuata, kila Mzanzibari atalipwa Sh500,000, hata mtoto atakayezaliwa siku hiyo, atapokea posho hiyo. Malipo hayo yatakuwa kila mwezi.

Ahadi nyingine ya Ameir ni kuwapa mikopo ya Sh10 milioni, kila mfanya-biashara mdogo, tena bila riba ili ku-wajengea uwezo wa mtaji.

Anasema akiwa Rais Zanzibar, Wazanzi-bari watakula mchele wa basmati peke yake. Kila ya basmati Zanzibar itakuwa Sh1,000.