Mgombea wa nafasi ya udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Ng’apa , Jimbo la Lindi Mjini Ndugu Issa Ngasha amewaomba wananchi wa kata hiyo kuiamini CCM na kuakikisha wanajitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Ng’apa katika uzinduzi rasmi wa kampeni uliofanyika tarehe 29 Septemba 2025.
Ngasha amesema wananchi wanapaswa kujitokeza kuchagua viongozi Kwani ni haki yao kikatiba na endapo yeye atachaguliwa na wananchi wa kata ya Ng’apa ataitumia nafasi hiyo kwa kufanya kazi kikamilifu katika kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi.
Pia Ngasha amewaomba wananchi wa kata hiyo Kumchagua Dkt Samia Suluhu Hassan ,Mbunge wa Jimbo la Lindi Mjini Mohammed Utaly ili waweze kuleta maendeleo.
Uzinduzi huo uliambatana na shamrashamra na hamasa kubwa kutoka kwa wanachaman wa CCM na wakazi wa kata hiyo, mgeni rasmi akiwa ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini , Jamadin Mandoa ambaye , aliwasihi wananchi kumuunga mkono Ngasha kwa kuwa ni kiongozi mwenye maono, uaminifu, na uzoefu wa kutosha.