INSPEKTA DK ONYANGO APEWA UBALOZI WA AMANI

Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey (wa pili kulia) akimfalisha joho, Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) baada ya kuhitimu masomo kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey (wa pili kulia) akimfalisha joho, Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) baada ya kuhitimu masomo kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey (wa pili kulia) akimkabidhi vyeti mbalimbali Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Ubalozi wa Amani, uliotolewa na Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Amani Duniani (United Nation University for Global Peace -UNUGP) kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.
Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango pamoja na wahitimu wengine akiwa kwenye hafla ya Mahafari yao yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey akizungumza kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Ubalozi wa Amani, uliotolewa na Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Amani Duniani (United Nation University for Global Peace -UNUGP) kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey (wa tatu kulia) akimkabidhi cheti Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Ubalozi wa Amani, uliotolewa na Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Amani Duniani (United Nation University for Global Peace -UNUGP) kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.

 Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango akiwa na wahitimu wengine kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.


 Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango akizungumza kukishukuru chuo chake mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Ubalozi wa Amani, uliotolewa na Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Amani Duniani (United Nation University for Global Peace -UNUGP) kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

CHUO Kikuu cha Umoja wa Mataifa cha Amani Duniani (United Nation University for Global Peace -UNUGP) kimemtunuku heshima ya kuwa Balozi wa Amani, Inspekta wa Polisi, Dk. Christina Onyango huku pia Chuo Kiuu cha LeadImpact cha Marekani kikimtunuku Shahada ya Uzamivu (PhD) baada ya kuhitimu masomo.

Wakati, chuo kikuu cha American University for Global Peace (AUGP-USA) kimemtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima na kufanya Onyango kuwa na shahada mbili za udaktari wa mbili za heshima katika eneo la utu. Kwa mara ya kwanza Onyango alitunukiwa shahada ya udaktari wa heshima mwaka 2020 na Chuo Kikuu cha LeadImpact.

Dk. Onyango ametunukiwa PhD hizo na Ubalozi wa Amani, kwenye Mahafari yaliofanyika katika Kanisa la Maisha ya Ushindi (VLC), Dar es Salaam, ambapo pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha LeadImpact, Profesa Cletus Bassey amewatunuku Mhitimu wa Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS), Elivia Fares na Jane Mbalingwa wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Shahada ya Udaktari ya Heshima ya Utu.

Profesa Bassey amempongeza Balozi Dk. Onyango huku akisisitiza ubora na umakini wa chuo hicho chenye matawi katika nchi mbalimbali duniani.

“Kwa LeadImpact, ili utunukiwe hata shahada ya heshima, lazima uwe umetimiza vigezo vyote kwa viwango vilivyopo na CV (wasifu) imepitiwa kwa umakini kwelikweli, hivyo nampongeza Inspekta Christina Onyango kwa kuyafanyia kazi aliyofundishwa na kuhitimu PhD na hata kutunukiwa heshima ya ubalozi wa Amani. 

Balozi Dk. Onyango aliyetunukiwa pia cheti cha Uchungaji Jamii, amelishukuru Jeshi la Polisi Tanzania kwa kumlea na kumsaidia hadi kufikia hatua ya kuwa balozi wa amani na kuahidi kuzidi kulitumikia kw weledi na uadilifu zaidi

“Namshukuru Mungu kwa kuwa balozi wa amani; si jambo dogo ndio maana sifa na utukufu namrudishia Mungu kwenye  kiti  chake cha enzi ,nazidi kunyenyekea sana ,mimi nipungue yeye azidi kuongezeka ndani yangu.”

“Pia namshukuru sana Afande IGP (Camillus Wambura), Afande Muliro (Kamanda wa Polisi, Kandaa Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro) na Afande RPC wangu (Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala) Afande Justino Mgonja na Afande  Mary Nzuki Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoti la Polisi Tanzania na Afande  Faidha ambaye ni ‘CO’ wa Dawati la Jinsia.wamenisaidia sana hadi kufika hapa. Kunitia moyo na kuniunga mkono kwa mambo mengi.”

Anaongeza: “Nawashukuru sana hao walezi wangu kwani bila wao nisingefika hapa na pia nashukuru Chuo Kikuu cha LeadImpact kwa Kozi ya Uchungaji na sasa mimi pia ni Mchungaji Jamii na pia nashukuru LeadImpact kwa kunitambua kuwa baozi wa amani maana sasa nimepewa uwanda mpana zaidi wa kuhudumia jamii nikiwa ndani ya Jeshi la Polisi.”

Akielezea safari yake hadi kuwa balozi wa amani na msomi wa ngazi ya udaktari, Balozi Inspekta Dk Onyango anasema mbele ya mahafari hayo: “Miaka mitano iliyopita (2020) nilitunukiwa udaktari wa heshima katika utu, namshukuru Mungu na leo nimetunukiwa PhD katika unasihi (Counselling) kama mhitimu maana nilipotunukiwa PhD ya heshima elimu yangu ilikuwa ni digrii ya kwanza…”

Anafahamisha: “Baada ya hapo, sasa nikaomba kusoma kabisa; LeadImpact wakanipa vigezo na masharti ikiwa ni pamoja na ama kusoma na kuhitimu masomo ya Master’s au kufanya na kufaulu mtihani wa kuhitimu master’s ndio maana miaka mitano yote napambana kwa ajili ya PhD… Kimsingi Chuo Kikuu cha LeadImpact si chuo cha kitoto; ipo kazi kwelikweli.”

Kwa mujibu wa Onyango, utafiti katika masomo yake ya PhD ulihusu vituo vya mkono kwa mkono maarufu, One Stop Center vinavyotoa huduma za pamoja na za haraka kwa waathirika wa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia vinavyojumuisha mwanasheria, askari polisi, daktarin na ofisa wa ustawi wa jamii ili kuhakikisha mwathirika anapata huduma za haraka bila kupoteza wala kuharibu Ushahidi.

Anaongeza: “Mimi mwenyewe nipo katika Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi Kivule katika Wilaya ya Kipolisi ya Ukonga Dar es Salaam. Kabla ya hizi One Stop Center, tulikuwa hatushindi kesi nyingi dhidi ya wahalifu wa ukatili wa kijinsia na mimi kama polisi nataka tunapofanya kesi dhidi ya mtuhumiwa ikithibitika awekwe hatiani.”

Anasema wakati anasoma, miongoni mwa mambo mengi makubwa aliyojifunza ni pamoja elimu ya namna ya kuwashinda wahalifu wa ukatili wa kijinsia na kuwa mnasihi (mshauri) wa kuleta mabadiliko kwa waathirika.

Balozi Dk Onyango anasema hadi kufanikisha azima hiyo, katika masomo yake na utafiti ameshirikiana na taasisi mbalimbali zikiwamo zinazopiga vita rushwa ya ngono na kutetea haki za binadamu na usawa wa kijinsia.

“Nazishukuru taasisi mbalimbali zikiwamo za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Nawashukuru  WilDAf,t TAWLA, WAJIKI na pia nashukuru  sana taasisi za elimu ya juu kama IFM, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mzumbe, Ardhi University na hata Wizara ya Afya walionipa ushirikiano mkubwa kwa kunipa takwimu zilizofanikisha utafiti wangu na hata in kuzunguka nao sehemu mbalimbali,”.  anasema.

Anaongeza: “Kwa kweli tumegundua na kusaidia wanafunzi wengi na hata wasio wanafunzi dhidi ya rushwa ya ngono ambayo ni tatizo kubwa na gumu katika jamii na wahusika wamechukuliwa hatua za kisheria.”

Kwa mujibu wa balozi huyo wa amani, kabla ya kuanzishwa One Stop Center miaka ya 2013, takwimu kuhusu matukio ya ukatili wa kijinsia zilikuwa juu, lakini kesi nyingi hazikuwa zikipata ushindi kuwatia hatiani wahalifu kama ilivyo sasa baada ya kuanzishwa vituo hivyo maana sasa kwa ukaribu na huduma zinazotolewa, ushahidi haupotei wala kuharibika kwa kuwa pia jamii inazidi kuelimishwa, waathirika wanafika vituoni mapema na kukutana na wahudumu wakiwamo polisi, daktari, mwanasheria na mtu wa ustawi wa jamii ndio maana sasa kesi nyingi zinapata ushindi.”