Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila amehukumiwa adhabu ya kifo na Mahakama ya Kijeshi ya nchini humo baada ya kupatikana na hatia ya makosa kadhaa ikiwemo ‘uchochezi’.
Kabila ambaye ana umri wa miaka 54 alifunguliwa mashtaka mnamo mwezi Juni kwa makosa ya uchochezi, uhalifu wa kivita na ushirikiano na kundi linalopigana na vikosi vya serikali Mashariki mwa nchi hiyo la M23.
Serikali mjini Kinshasa inamshutumu Kabila kwa kushirikiana kwa ukaribu na Rwanda pamoja na kundi la waasi la M23 ambalo limeiteka miji muhimu Mashariki mwa Kongo.
Mnamo mwezi Mei Bunge la Seneti la nchi hiyo liliondoa kinga ya kisheria dhidi yake, hatua ambayo Kabila aliikosoa na kuiita ya kidikteta.
Related