TRA YAMKABIDHI BI. ZAINAB SH. MILIONI 2 ILI AFUFUE BIASHARA YAKE

:::::                                                                   Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imemkabidhi kiasi cha Sh. Milioni Mbili (2,00,000) Bi. Zainab Msamehe mkazi wa Tegeta mkoani Dar es Salaam kwaajili ya kufufua biashara yake ambayo ilikuwa imekufa.

Fedha hizo zimekabidhiwa Septemba 30.2025 na Meneja TRA Mkoa wa Kikodi Tegeta Bw. Dickson Qamara kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda, kiasi ambacho kimetolewa kwa lengo la kumuwezesha kuanza upya baishara zake baada ya mtaji wake kuanguka.                                              

Bw. Mwenda alifanya uamuzi wa kumpatia mtaji Bi. Zainab wakati akizindua dawati la uwezeshaji biashara mkoa wa Dar es Salaam lililozinduliwa Septemba 27.2025 katika viwanja vya Mnanzi mmoja akiwa ni mgeni rasmi wa tukio hilo.                                                                     Kwa upande wake Bi. Zainabu ameishukuru TRA kwa kuanzisha dawati hilo, kuweza kumpatia TIN na Kamishna Mkuu kumpatia kiasi hicho cha fedha ili kuanza tena biashara zake.

Bi. Zainab alitoa wito kwa watu wote kuwa na ukaribu na TRA na kutumia vizuri dawati hilo la uwezeshaji biashara kwania ya kujifunza na kulipa kodi zao vizuri.

= = = = =