Yanga Warejea Dar Baada Ya Kulazimishwa Sare Na Mbeya City – Global Publishers

Kikosi cha Yanga SC kimewasili jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Septemba 30, 2025, ambapo walitoka suluhu ya bila kufungana na wenyeji Mbeya City.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulimalizika kwa matokeo ya Mbeya City 0–0 Yanga SC, hali iliyowafanya mashabiki wa Yanga kusubiri kwa hamu kurejea kwa ushindi kwenye michezo ijayo.

Baada ya kurejea Dar, Yanga inatarajia kuendelea na maandalizi ya mechi zinazofuata za Ligi Kuu na pia michuano ya kimataifa, huku benchi la ufundi likiahidi kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo huo wa Mbeya.