ZITTO KABWE ANADI MGOMBEA UBUNGE KIGAMBONI KUPITIA ACT WAZALENDO

 :::::::::

Kiongozi wa Chama Mstaafu cha ACT Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe, leo tarehe 2 Oktoba 2025, amefanya ziara maalum katika Jimbo la Kigamboni kwa ajili ya kumnadi rasmi mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Wakili Mwanaisha Mndeme.

Katika ziara hiyo, Ndugu Zitto amekutana na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wavuvi, wamachinga, na madereva wa bodaboda, akisikiliza changamoto zinazowakabili na kueleza mipango ya ACT Wazalendo katika kutatua matatizo hayo kupitia sera za mabadiliko ya kweli.

Ziara hiyo imehitimishwa kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Kata ya Kimbiji, ambapo viongozi wa chama na mgombea walitoa maelezo ya kina kuhusu dira ya ACT Wazalendo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Wakili Mwanaisha Mndeme ameahidi kuleta uwakilishi imara na wa kweli kwa wananchi wa Kigamboni.

Kupitia ziara hii, wananchi wa Kigamboni wamepata fursa ya kusikiliza sera mbadala zinazolenga kuondoa changamoto za muda mrefu na kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

ACT Wazalendo inaendelea kusimama kidete kwa ajili ya usawa, uwajibikaji, na maendeleo jumuishi kwa Watanzania wote.