WADAU wote wa Sekta ya Usafirishaji hususani watoa huduma wa Malori ikiwemo Wamiliki Madereva na Wauzaji wa Vifaa pamoja mafundi wametakiwa kuhakikisha Wanaimarisha Usalama wa huduma wanayoitoa ili kudhibiti ajali za barabarani zinazotokea.
Agizo Hilo amelitoa Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TAMSTOA) Chuki Shaban Jijini Dar es salaam Wakati akifanya Uzinduzi wa Kampuni inayojihusisha na Uuzaji wa Vipuli vya Malori ya Kichina ‘Samol automotive’ ambapo ametoa pongezi kwa Wadau hao kusogeza huduma hiyo hapa Tanzania.
“Huduma zenu mzitoe kwa Uhakika na kutoa Ushauri wa kitaalamu kwa wateja wenu na ninatambua mchango wenu Samol Automotive katika utoaji wa Vipuli halisii vyenye ubora vyenye viwango vya kukidhi mahitaji ya Soko hivyo tumieni mtandao ya kijamii kutoa Elimu matumizi salama ” Amesema
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Samol Automotive Aboul Wahab Sariko Amesema 2010 Magari ya Kichina yalikuwa ni 10% katika Soko la Afrika lakini kwa sasa imefikia 55%hivyo wao waliamua kuuza na kusambaza Vipuli vya Malori ili kusaidia kurahisisha upatikanaji wake mafundi na Madereva na Magari yanapoharibika wasitumie muda mrefu kutafuta na wanauza Vifaa vyenye viwango Bora.
” Kampuni yetu ilianzishwa Mwaka 2023 na Sisi kimsingi tunajishughulisha na Uuzaji usambazaji na vizuri vya Malori ya kichina ikiwemo Fau Houw,Chakman Sisi tuliamua kufanya shughuli hii kutokana na Ongezeko la Magari ya Kichina katika Soko la Afrika” Amesema Mkurugenzi
Hata hivyo pia Amesema wanauza Malori ya kichina hivyo wamechagua eneo la Tabata Matumbi kutokana na eneo hilo kuwa ndiyo kitovu cha Wauzaji Vifaa vya Malori Makubwa yote.