::::::
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limeandaa wiki maalum ya huduma kwa wateja itakayofanyika kuanzia Oktoba 13 hadi 19, 2025 katika ofisi zake za Bamaga, jijini Dar es Salaam.
Katika kipindi hicho, huduma mbalimbali zitatolewa papo kwa papo kwa wateja, ikiwemo kupatiwa vyeti mbadala kwa waliopoteza, huduma ya D2 Uthibitisho wa Matokeo, pamoja na DE Ulinganifu wa Vyeti (Equivalence).
Lengo la wiki hiyo ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kurahisisha upatikanaji wa nyaraka muhimu zinazotolewa na Baraza hilo.