Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Manyara
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na maendeleo makubwa ya yaliyofanyika kwa wananchi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara katika sekta za maendeleo ya jamii maji, umeme, elimu na afya pia yamefanyika na maeneo mengine ya Tanzania nzima.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara akiwa katika mkutanoNE wa kampeni kuomba kura kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu,Dk.Samia amesema Serikali ya CCM imefanyakazi ya maendeleo katika nchi nzima.
“Tumekuja kwenu Hanang kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi Kuja kuwaambia tulivyowajibika miaka mitano iliyopita na tutakavyowajibika mkitupa ridhaa miaka mitano inayokuja.
“Kwa hapa Wiilaya ya Hanang tumejenga stendi ya mabasi ya kisasa inayofungua fursa za biashara na niwaombe sana stendi ile siyo kupanda na kushuka kwenye magari bali ni eneo la biashara hivyo tumieni kufanyabiashara kukuza uchumi.”
Pia Mgombea urais kupitia CCM Dk.Samia amesema serikali itaendelea kujenga miundombinu ya barabara na miongoni mwa barabara hizo ni Nangwa – Isambala – Kondoa kilometa 79 ambayo itajengwa kwa lami.
Vilevile barabara ya Mogito – Hydom kilometa 70 itajengwa kwa kiwango kitakachopitika mwaka mzima.
Kuhusu sekta ya mifugo amesema Serikali katika miaka mitano iliyopita imefanikiwa kuwajengea wafugaji majosho matano na machinjio matatu huku pia akisisitiza imeendelea adha na zoezi la chanjo kwa ruzuku pamoja na utambuzi wa mifugo.
Dk. Samia amesema Serikali inatekeleza mpango huo kwani Tanzania imefanikiwa kupata soko la nyama na wanyama hai.
Hata hivyo, amesema Tanzania ilikumbana na changamoto ya mifugo kutochanjwa hivyo kutokuwepo katika rekodi ya dunia namna nchi inavyofuatilia mifugo yake.
Kwa sababu hiyo, amesema Serikali imelazimika kutoa chanjo hiyo kwa bei ya ruzuku ili soko litakapopatikana kila mfugaji atakakuwa na cheti cha utambuzi wa mifugo yake kuchanjwa.
“Tuna soko mpaka hatuwezi kulimaliza kwa hiyo ndugu zangu wafugaji kazi ni kwenu soko lipo endeleeni na kazi.Ilikukuza biashara ya mifugo, Serikali imefanya ukarabati minada ya Kateshi, Masodeshi na Hendagau.”
Dk.Samia amesema kuwa minada hiyo imefanyiwa ukarabati ambapo sasa hata mtu kutoka nje ya nchi kununua wanyama hai anaweza kununua bila wasiwasi.