TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Zambia.
Mchezo huo ni maalumu kwa ajili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2026 unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar,
Tayari kikosi kimetajwa kwa ajili ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 4:00 usiku. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka la Tanzania, (TFF) alibainisha kuwa baada ya mchezo huo kikosi kitaelekea Dubai.
Dubai watakwenda kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran ambapo amebainisha kuwa wanauchukulia mchezo huo kwa uzito mkubwa.
“Baada ya kikosi kutajwa kuelekea kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Zambia, wachezaji wataripoti kambini Oktoba 4. Bado ni mchezo muhimu kwetu tunahitaji alama zaidi kwa hiyo tunauendelea mchezo huo kwa umakini.
“Baada ya mchezo wetu dhidi ya Zambia kikosi kitasalia Zanzibar kwa siku mbili ambapo tutakuwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao upo kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Iran Oktoba 14, Iran ni moja ya timu 21 ambazo zina ubora hivyo ni mchezo ambao tunauchukulia kwa uzito mkubwa,” amesema Ndimbo.
Tayari kikosi cha Taifa Stars kimeitwa ambapo miongoni mwa wachezaji hao ni Yakoub Suleman huyu ni mlinda mlango wa Simba SC, Hussein Masalanga wa Singida Black Stars, Zuber Foba wa Azam FC, Israel Mwenda wa Yanga SC na Feisal Salum wa Azam FC chini ya Kocha Mkuu, Hemed Suleman.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.