Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na Chama cha mchezo wa Gofu Tanzania (TGU), kimewakutanisha jumla ya wachezaji 150 wa mchezo huo, kutoka mataifa zaidi ya nane Duniani, shabaha kuu ikiwa ni kuendelea kuongeza ushindani wa mchezo wa gofu nchini na baadaye kimataifa kupitia mchezo huo.
Timu ya uongozi wa Vodacom ikiongozwa na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi David Tarimo na Afisa Mtendaji Mkuu Philip Besiimire wakifungua mashindano ya golf ya Vodacom Tanzania Open 2025 ikiwa ni siku ya tatu ya mshindano hayo , yenye lengo la kuendeleza mchezo wa golf nchini ambapo kampuni hiyo imesimama kuwa mdau mkua anayechangia ukuaji wa mchezo huo ikishirikiana na chama cha golf Tanzania . Tukio limefanyika leo jijini Arusha.