*Watu milioni 14.6 wamehudhuria katika mikutano yake ya kampeni.
*Wengine milioni 31.1 wamefuatilia kupitia vyombo mbalimbali vya habari
*Sababu mikutano yake kufurika wananchi yatajwa, Oktoba 7 kuanza Kanda ya Ziwa
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Dodoma
KATIBU wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi amesema tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu mgombea wao wa Urais Dk.Samia Suluhu Hassan tayari ameshafanya mikutano katika mikoa 21 ambapo watu milioni 14.62 wamehudhuria katika mikutano yake na watu milioni 31.6 wamefuatilia kupitia vyombo vya habari.
Akizungumza leo Oktoba 5,2025 Mjini Dodoma wakati anatoa tathimini ya mikutano ya kampeni za mgombea urais Dk.Samia , Kihongosi ameeleza leo Oktoba 5 ni siku ya 39 tangu walipozindua kampeni za chama chao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
“Sote tutakuwa tunaikumbuka Agosti 28, 2025, tulipofanya uzinduzi wa mikutano ya kampeni, uliofanyika Viwanja vya Tanganyika
Packers, Kawe, Dar es Salaam. Mutano huo ulivunja rekodi ya mahudhurio na shamrashamra kuwahi kutokea katika historia chama chetu.
“Tangu mutano huo, mgombea wetu wa urais, Dkt Samia Suluhu Hassan, ameshafanya mikutano 77, katika mikoa 21, kwenye kanda za Kati, Magharibi, Pwani, Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Pemba na Unguja (Zanzibar), vilevile Kanda ya Kaskazini. Zaidi ya watu milioni 14.62 wamejitokeza kwenye mikutano moja kwa moja.
“Pia watu milioni 31.6, wamefuatilia kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Mikutano yote hiyo, kanda kwa kanda, mkoa hadi mkoa, mahudhurio yamekuwa makubwa.Hiyo ni kuonesha jinsi mgombeawetu wa urais, Dkt Samia Suluhu Hassan,anavyokubalika, na wananchi kwa mamilioni, wameweka imani kubwa kwake.”
Akiendelea kutoa tathimini hiyo Kihongosi amesema imani ya wananchi kwa Dk. Samia Suluhu Hassan, siyo bahati wala mkumbo, bali ni imechagizwa na ongozi wenye mafanikio makubwa katika miaka minne aliyoshika usukani wa urais.
“Dk.Samia alipoingia madarakani alipokea mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (INHPP), ukiwa asilimia 37 hadi kufikisha asilimia 99.55. Mradi huo umekamilika na watanzania wanafurahia matunda ya mradi huo ambao unazalisha umeme.”
“Pia Dk.Samia amefanya vema kwenye miradi ya miundombinu, kuanzia Reli ya Standard Gauge (SGR), kutoka Dar es Salaam mpaka Makutupora (kilometa 722), kisha mapinduzi makubwa ya usafiri wa treni kati ya. Dar es Salaam na Dodoma. Sasa hivi, Shirika la Reli Tanzania (TRC), lina vichwa vya treni 17 na mabehewa 67
“Wananchi wanajionea kasi ya ujenzi wa miundombinu ya SGR, kutoka Makutupora kwenda Tabora hadi Isaka, halafu Isaka maka Mwanza, Tabora kwenda Kigoma, vilevile Uvinza hadi Musongati.
“Ndani ya miaka minne ya ongozi wake, Dk. Samia amejenga kilometa 15,366.36.Chini ya ongozi wa Dk Samia, ndege mpya sita za abiria na moja ya mizigo, zimenunuliwa, hivyo kufanya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kuwa na ndege 16.
“Wananchi wa Tanzania, hasa wa vijijini wamekuwa mashuhuda wa kazi kubwa ya Rais Samia. Miradi 1,633 ya usambazaji wa maji imekamilika, miongoni mwa hiyo, miradi 1,335 ni ya vijijini peke yake.”
Akiendelea kueleza amesema katika sekta ya afya, ndani ya miaka minne ya Dk. Samia, vituo vipya vya afya 1,368 vimejengwa, hospitali zinazotoa huduma za dharura (EMD), zilikuwa saba nchi nzima wakati Dk. Samia anashika madaraka, sasa zipo 116.
Pia vituo 183 vyenye uwezo wa kutoa huduma za uzazi ikiwemo upasuaji, vimejengwa.
Katika sekta ya elimu, shule za msingi zimeongezeka hadi kufikia 19,783, kutoka 16,656, wakati Dk Samia anaingia madarakani.” Shule za sekondari zimefikia 5,926 kutoka 5,001, Bajeti ya mikopo ya elimu ya juu imeongezekana kutoka Shilingi bilioni 464 mpaka bilioni 786,”amesema Kihongosi.
Kwa upande wa uchumi wa nchi umekua kwa kasi, kutoka asilimia 3.9, Dk. Samia
aliposhika madaraka, hadi asilimia 5,5 mwaka 2024. Matarajlo ni kufikia asilimia 6 mwaka huu 2025.
Kuhusu ajira amesema ajira milloni 8 zillitengenezwa miaka minne ya Dkt Samia, miaka mitano ijayo matarajlo ni ajira na Utu ni falsafa ya Dkt Samia, na alianza kuitekeleza kwa kuwapa nyongeza mishahara na kupandisha madaraja wafanyakazi, kipindi ambacho wafanyakazi walikuwa wamesimama bila kuongezewa mishahara kwa miaka saba.
“Hayo ni sehemu ya mambo mengi ambayo yanawafanya wananchi kujitokeza kwa wingi. Upekee wa Dkt ni ahadi zake ambazo zinagusa moja kwa moja maisha ya Watanzania.
“Kuna marufuku ya kuzuia maiti hospitali kwa sababu ya bili za matibabu, bima ya afya kwa wazee, watoto na walemavu, wagonjwa wa saratani, kisukari na figo kutibiwa bure, kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya ndani siku 100.
“Pia kutoa Shilingi bilioni 200 kwa wafanyabiashara wadogo ili kuwainua kimtaji, ajira mpya za walimu na wahudumu wa afya. Pamoja na ahadi nyingie, ni mambo ambayo yanawavutia Watanzania kupenda kumsikiliza Dk. Samia.”
Kihongosi amesema “Tunapotazama kalenda leo, Oktoba 5, 2025, zimebaki siku 24 kufanyika Uchaguzi Mkuu. Mgombea urais wetu, Dk Samia Suluhu
Hassan, ataanza ziara yake ya kampeni Kanda ya Ziwa, yenye mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita, Mara na Kagera.
“Matarajio ni kwamba mikutano ya mgombea urais wetu itaendelea kufanya vizuri kwa sababu ya mafanikio yaliyopatikana kwenye kanda hiyo chini ya ongozi wake.
“Kukamilika kwa Daraja la Busisi (Daraja la Magufuli), kukamilika kwa ujenzi wa chanzo cha maji cha Butimba, kinachowanufaisha wananchi 450,000 Mwanza. Kufanikiwa kwa mradi wa maji ya Ziwa Victoria, unawahudumia wananchi 86,980 wa Tinde na Shelui.”
Ameongeza kuwa ujenzi wa vivuko sita Ziwa Victoria vimekamilika na kuanza kazi sambamba na uwepo wa boti ya kuhudumia majeruhi wa ajali (Ambulance), Ziwa Victoria. Chanjo ya mifugo imezinduliwa na Sh. bilioni 62 imetolewa.
“Hayo na mengine yaliyofanyika, Dkt Samia bado ana fungu la neema kwa watu wa Kanda ya Ziwa. Muhimu wajitokeze kumsiiliza kuanzia Oktoba 7, 2025.”